Home / Habari Za Kitaifa / SMZ YAIPONGEZA CUBA MISAADA SEKTA YA AFYA.

SMZ YAIPONGEZA CUBA MISAADA SEKTA YA AFYA.

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema imeridhishwa na misaada inayotolewa na Serikali ya Cuba katika sekta mbalimbali ikiwemo ya afya ambayo imeongeza idadi ya wataalamu nchini.

Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati alipozungumza na balozi wa Cuba ambaye amemaliza muda wa kazi nchini.

Balozi Iddi alisema sekta ya afya imepata mafanikio makubwa Zanzibar kwa kutoa wahitimu ambao wamekuwa wakifanya kazi katika kutoa huduma za afya katika hospitali mbalimbali nchini.

Alisema hatua hiyo imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la madaktari nchini lililokuwepo awali katika hospitali zilizopo Unguja na Pemba.

Awali, Balozi wa Cuba anayemaliza muda wake wa kazi nchini, Jorge Luis Lopez alisema nchi yake ni moja ya marafiki wakubwa wa maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo afya.

Alisema Cuba inajivunia kuona Zanzibar imepata mafanikio makubwa katika sekta ya afya na hivyo katika kipindi kifupi kujitosheleza na wataalamu hao. Alisema anaondoka nchini huku akiridhishwa na hali ya amani na utulivu pamoja na maendeleo makubwa yanayopatikana katika visiwa vya Unguja na Pemba.

SOURCE HABARI LEO.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *