Home / Habari za Kimataifa / NETANYAHU AMUOMBEA MSAMAHA MWANAJESHI ALIYEUA ISRAEL.

NETANYAHU AMUOMBEA MSAMAHA MWANAJESHI ALIYEUA ISRAEL.

Netanyahu kitendo hicho kilifanywa bila kukusudiwa

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema anaunga mkono wito wa msamaha kwa mwanajeshi wa Israel aliyekutwa na hatia ya kuuwa bila kukusudia baada ya kumpiga risasi mshambuliaji wa Palestina aliyekutwa amelala chini akiwa na majeraha.

Waendesha mashtaka wamesema mauaji hayo yaliyotekelezwa na Elor Azaria Magharibi mwa benki iliyokuwa na watu wengi yalikuwa ni kitendo cha kulipiza kisasi.

Lakini viongozi mashuhuri katika Baraza la Mawaziri la bwana Netanyahu wamekosoa maamuzi hayo, ingiwa baba wa Raia huyo wa Palestina alisema maamuzi hayo yalikuwa yenye haki.

Mashtaka haya yameleta utengano mkubwa katika jamii ya Israel.

Azaria amejitetea kuwa alikua anajihami katika tukio hilo

Jeshi limesema Sergeant Azaria amekiuka kanuni za maadili ya kijeshi lakini wanaomuunga mkono wanasema mwanajeshi huyo alikuwa anajilinda na kwamba viongozi wake wamemgeuka.

SOURCE BBC SWAHILI.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *