Home / Habari Za Kitaifa / DHAMANA YA LEMA MAHAKAMA YA RUFAA.

DHAMANA YA LEMA MAHAKAMA YA RUFAA.

HATIMA ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema sasa iko mikononi mwa Mahakama ya Rufaa baada ya jana mawakili wa serikali kuwasilisha maelezo ya notisi ya kukusudia kukata rufaa kupinga mbunge huyo kupewa dhamana.

Msuguano wa kisheria kati ya mawakili wa Lema na wa serikali umedumu kwa zaidi ya miezi miwili sasa huku kila upande ukipinga uamuzi ya upande mwingine.

Mawakili wa serikali waliwasilisha notisi hiyo iliyosajiliwa Desemba 30, mwaka jana katika masjala ya Mahakama ya Rufaa Kanda ya Arusha na itapangiwa tarehe katika vikao vya mahakama hiyo vinavyokaa mara tatu kwa mwaka.

Lema alikamatwa mjini Dodoma Novemba 2, mwaka jana na kufikishwa mahakamani Novemba 8 mwaka huo huo kwa mashitaka ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.

Alinyimwa dhamana na kurudishwa mahabusu katika Gereza la Kisongo lililopo nje kidogo ya Jiji la Arusha. Jana Jaji Salma Magimbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, alitarajiwa kusoma uamuzi wa ama kumpa Lema dhamana au la, kufuatia ombi la notisi ya kupinga dhamana lililowasilishwa na mawakili wa Serikali mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Desderi Kamugisha, Novemba 11 mwaka jana.

Katika ombi hilo, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Paul Kadushi, aliwasilisha notisi ya kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga Lema kupewa dhamana, ombi ambalo alilitamka muda mfupi kabla ya Hakimu Kamugisha kutoa masharti ya dhamana.

SOURCE HABARI LEO.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *