Home / Habari za Kimataifa / MKUTANO KUTATUA MZOZO KATI YA ISRAEL NA PALESTINA WAFANYIKA UFARANSA.

MKUTANO KUTATUA MZOZO KATI YA ISRAEL NA PALESTINA WAFANYIKA UFARANSA.

Mkutano kati ya Israel na Palestina hujafanyika tangu 2014

Mawaziri wa mashauri ya nchi za kigeni na wanadiplomasia wa zaidi ya mataifa sabini wanakutana mjini Paris, Ufaransa, kwa mkutano maalum kujadili mzozo na suluhu ya kudumu kati ya Israel na Palestina.

Hakuna wajumbe kutoka Israel au Palestina, ambao wanahudhuria mkutano huo.

Waandalizi kutoka Ufaransa, wanasema kwamba ni bora kuwekwa katika madaftari ya kumbukumbu, kwamba sulu katika mataifa hayo mawili, ni msingi wa siku zijazo wa muafaka wa amani.

Hayo yanatukia, licha ya msimamo mkali wa Marekani dhidi ya Israeli wakati ambapo Rais mpya Donald Trump anajiandaa kuchua uongozi.

Waziri mkuu wa Israeli, Bejamin Netanyahu, anaelezea mkutano huo kama mabaki ya kale.

Wanajeshi wa Israel na Palestina hukabiliana mara kwa mara
 
Mazungumzo ya amani yamekwama kutokana na ujenzi wa makaazi ya wayahudi
SOURCE BBC SWAHILI.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *