Home / Habari za Kimataifa / DEWJI AWANIA TUZO ZA ALM.

DEWJI AWANIA TUZO ZA ALM.

Mohamed Dewji

Zoezi la kuchagua mshindi wa tuzo ya ALM 2016 lafungwa, MO Dewji aongoza kwa asilimia 60.8

Jarida la African Leadership limefunga zoezi la kupiga kura kuchagua mshindi wa tuzo ya African Leadership Magazine Person Of The Year 2016, tuzo ambazo Mtanzania Mohammed Dewji alikuwa mmoja kati ya watu nane ambao walikuwa wakiwania.

Baada ya kufungwa kwa zoezi hilo, Mohammed Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) ameibuka mshindi baada ya kuongoza kwa asilimia 60.8.MO Dewji ameongoza kwa kupata kura nyingi na akifuatiwa na Rais Mstaafu wa Ghana, John Mahama ambaye amepata asilimia 38.3.

Kwasasa bado Jarida la African Leadership hawajatoa taarifa ni lini watakabidhi tuzo kwa mshindi wa wa tuzo ya African Leadership Magazine Person Of The Year 2016.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *