Home / Michezo / Mwanamiereka wa WWE Jimmy ‘superfly’ Snuka afariki dunia

Mwanamiereka wa WWE Jimmy ‘superfly’ Snuka afariki dunia

Jimmy Snuka

Mwanamiereka wa WWE,Jimmy Snuka alimaarufu kama ‘Superfly’ amefariki akiwa na umri wa miaka 73.

Wakili wake amesema mwanamiereka huyo aliaga dunia akiwa katika nyumba ya mkwe wake mjini Florida, akiwa pamoja na familia yake.

Mzaliwa huyo wa Fiji alikuwa wakati mwingi hospitalini kwa shida tofauti ikiwemo ugonjwa wa kiakili wa Dementia, lakini chanzo cha kifo chake bado hakijabainika

Katika taarifa kwenye mtandao wa shirika la WWE imesema imesikitishwa na kifo kilichompata ‘mwanzilishi wa kitengo cha high flying’ katika ukumbi wamiereka.

Mtoto wake Tamina Snuka, pia nyota wa miereka, aliandika kwenye mtandao wa Twitter, ‘Nakupenda babangu’ na kuambatisha picha yake na babake kwenye ujumbe wake huo.

Ni chini ya wiki mbili tangu, mashtaka ya mauaji kutupiliwa mbali dhidi yake kuhusiana na kifo cha mpenzi wake mwaka 1983.

Jaji alitoa uamuzi huo baada ya kubaini Jimmy alikuwa na upungufu wa kiakili na hangeweza kuendelea na kesi hiyo ya mauaji ya mpenzi wake Nancy Argentino.

Mashtaka hayo waliwasilishwa mahakamani mwaka 2015.

Alikana madai hayo ya mauaji.

Nyota wa miereka wamekuwa wakituma risala za rambirambi kwa Snuka kwenye mitandao ya kijamii.

SOURCE BBC SWAHILI.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *