Home / Habari za Kimataifa / NDEGE YA JESHI YAUA KIMAKOSA TAKRIBAN WATU 50 NIGERIA.

NDEGE YA JESHI YAUA KIMAKOSA TAKRIBAN WATU 50 NIGERIA.

Rubani wa ndege kimakosa aliamini kuwa alikuwa akiwashambulia wapiganaji.

Ndege ya jeshi la Nigeria imewaua kimakosa raia na kuwajeruhi wengine katika eneo la Rann kaskazini mashariki mwa nchi.

Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka MSF, linasema kuwa takriban watu 50 wameuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa

Wafanyakazi wa kutoa misaada ni baadhi ya wale waliouawa huku shirika la msalaba mwekundu likisema kuwa 6 kati ya wafanyakazi wake waliuawa.

Shambulizi hilo lilitokea karibu na mpaka wa Nigeria na Cameroon ambapo jeshi la Nigeria limekuwa likipigana na kundi la Boko Haram.

Msemaji wa jeshi Meja Jenerali Lucky Irabor, anasema kwa rubani wa ndege kimakosa aliamini kuwa alikuwa akiwashambulia wapiganaji.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, ametuma rambi rambi akisema kuwa amehusunishwa na kupotea kwa maisha na kuomba kuwepo utulivu.

MSF inasema kuwa watu wengi waliouawa ni wale waliohama maeneo ambapo Boko Haram walikuwa wemeendesha mashambulizi.

SOURCE BBC SWAHILI.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *