Home / Habari za Kimataifa / URUSI NA UTURUKI WAFANYA MASHAMBULIZI YA PAMOJA SYRIA.

URUSI NA UTURUKI WAFANYA MASHAMBULIZI YA PAMOJA SYRIA.

Urusi ina ndege katika kituo cha Hmeimim kilicho nchini Syria

Urusi na Uturuki zimefanya mashambulizi yao ya kwanza ya pamoja, dhidi ya kundi la Islamic State nchini Syria, kwa mujibu wa wizara ya ulinzi nchini Syria.

Islamic State ililengwa katika vitongoji vya mji wa al-Bab mkoani Aleppo, ambapo Uturuki ilikumbwa na maafa makubwa mwezi uliopita ikipigana na Islamic State.

Msemaji wa Urusi Luteni Sergei Rudskoi amesema kuwa mashambulizi hayo ya pamoja yamekuwa yenye mafanikio makubwa.

Urusi na Uturuki wamengilia pakubwa vita vya Syria.

Mji wa al-Bab ulio umbali wa kilomita 20 kutoka mpaka wa Uturuki, umekuwa ukilengwa na harakati za Uturuki zenye lengo la kuwatimua wanamgambo wa Islamic State na vikosi vya Kurdi.

Ndege za Marekani nazo ziliendesha mashambulizi mapema wiki hii pia kwa ushirikiano na Uturuki.

Ndege za Uturuki za F-16 zilishiriki

SOURCE BBC SWAHILI.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *