Home / Habari Za Kitaifa / WAPIGA ‘DILI’ BANDALINI KUFILISIWA.

WAPIGA ‘DILI’ BANDALINI KUFILISIWA.

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema itawachukulia hatua watumishi wa mamlaka hiyo wote ambayo wanajishughulisha na michezo michafu wakishirikiana na wafanyabiashara katika minada inayofanyika bandarini.

Akizungumza katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo cha redio jana, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedit Kakoko amesema hatua ambazo atachukua ni pamoja na kupiga mnada mali za wahusika wote ambao watabainika kuhusika katika mchezo huo mchafu.

“Katika Serikali ya Awamu ya Tano ni vizuri kufuatilia utendaji, kilichozungumzwa tumekisikia na tuko tayari kuchukua hatua za haraka kwa kinachozungumzwa,” alisema Kakoko.

Kakoko amesema, anatambua kuwa kuna minada inafanyika katika Bandari ya Dar es Salaam kwa mizigo ambayo hushindwa kulipiwa ndani ya muda uliowekwa kisheria, lakini hakuwa na taarifa ya njama zinazofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa TPA ambao sio waaminifu, “Kama tukipata taarifa za kina tutachukua hatua mara moja,” alisema.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa hiyo ambaye ni mdau wa bandari, kuna ujanja unaofanywa na baadhi ya wafanyakazi ambao wanaagiza mzigo kutoka nje, wanalipia asilimia chache kwa makubaliano kwamba mzigo huo utakapofika bandari ya Dar es Salaam atamalizia fedha zilizobaki.

Lakini wafanyabiashara hao matokeo yake wakifikisha mzigo hapa nchini badala ya kulipa fedha zilizobaki wanachelewesha kulipia mzigo mpaka muda unapita wa kuhifadhi mzigo bandarini na mzigo huo kupigwa mnada.

Aidha, mchezo huo mchafu hufanywa na wafanyakazi wasio waaminifu wa TPA kwa kushirikiana na wafanyabiashara kisha mzio anauziwa kwa bei ya chini ambapo bila kulipa fedha ambayo mfanyabiashara alikuwa amebakiza deni alikochukulia mzigo jambo ambalo linachafua jina la bandari ya Dar es Salaam.

SOURCE HABARI LEO.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *