Home / Habari za Kimataifa / ITALIA: WATU 8 WAOKOLEWA KUTOKA JENGO LILILOZIKWA KWENYE BARAFU.

ITALIA: WATU 8 WAOKOLEWA KUTOKA JENGO LILILOZIKWA KWENYE BARAFU.

Helikopta ziliitwa kwenye eneo la tukio mahala ambapo wmanusura walipatikana

Watu wanane wamepatikana wakiwa hai katika hoteli ya Italia-Rigopiano hotel, siku mbili baada ya kuzikwa katika theruji kubwa.

Waokoaji wanasema manusura hao sita wamebainika wakiwa wamezikwa chini ya theruji ,lakini walikuwa bado hawajaokolewa.

Mmoja wapo ni msichana mdogo, vimesema vyombo vya habari vya Italia.

” Wako hai na tunaongea nao,” msemaji wa kikosi cha zima moto Luca Car alilieleza shirika la habari la Rheuters.

Barafu yenye kina kikubwa iliizika hoteli hiyo iliyopo eneo la mbali katika jimbo la kati la Abruzzo , baada ya matetemeko kadhaa ya ardhi kulikumba eneo hilo.

Takriban watu wanne wamethibitishwa kufa kwenye mkasa huo na wengine wapatao 20 hawajulikani walipo, huku juhudi za uokozi zikiendelea katika hali ngumu na mbaya ya hewa.

Watoto wanaaminiwa kuwa miongoni mwa wageni waliokuwemo kwenye hoteli mkasa huo ulipotokea

Watoto wanaaminiwa kuwa miongoni mwa wageni waliokuwemo kwenye hoteli mkasa huo ulipotokea.

Timu za uokoaji zimekuwa zikiendelea na kazi ya kuwasaka manusura na miili ya wahanga wa mkasa huo kwa zaidi ya saa 24 huku kiwango cha joto kikiwa ni chini ya nyuzi joto sifuri.

Vikosi vya uokozi vimeomba usaidizi wa helikopta ili kuwaokoa watu wanane waliopatikana hai, kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya Italia.

Hoteli ilikuwa imezikwa kabisa ndani ya barafu kwa saa kadhaa kabla timu ya waokoaji haijafika kwenye eneo la tukio reached the scene

Mnamo siku ya Jumatano matetemeko ya ardhi yakiwemo manne yenye ukubwa wa zaidi ya 5 kwa vipimo vya ritcha, yaliyokumba jimbo hilo ambalo tayari linakabiliwa na heruji nzito ambayo ilizika mifumo ya mawasiliani ya simu na kuharibu nyaya za umeme.

Milingoti ya simu ilianguka katika hoteli ya Rigopiano mapema Jumatano.

Baadhi ya taarifa zinasema kuwa wageni walikuwa wamekusanyika katika ukumbi wa chini wa gorofa ya hoteli wakisubiri kuokolewa kufuatia matetemeko ya ardhi.

Wamekaa kwa saa kwa saa 40 chini ya vifusi katika barafu na vifusi vya jengo.

SOURCE BBC SWAHILI.

 

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *