Home / Michezo / ‘Simba SC bahati yao’

‘Simba SC bahati yao’

NAHODHA wa Mtibwa Sugar, Shabaan Nditi amesema ubovu wa uwanja umesababisha kucheza chini ya kiwango na kutoka suluhu na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Akizungumza na gazeti hili, Nditi ambaye amewahi kuchezea Simba kabla ya kwenda Uarabuni na kurudi Mtibwa Sugar, alisema wanafanya mazoezi kwenye uwanja mzuri, lakini kwenye mechi wamecheza Uwanja wa Jamhuri ambao sehemu ya kuchezea ni mbovu.

“Uwanja umesababisha tushindwe kucheza vizuri na ilikuwa ukisubiri mpira udunde unapoteza uelekeo, hivyo tumeshindwa kufikia lengo la kuifunga Simba,” alisema Nditi.

Nahodha wa Simba, Jonas Mkude alisema wanakubaliana na matokeo kwani kwenye mchezo kuna matokeo matatu na kuahidi kufanya vizuri kwenye mechi zijazo.

Suluhu hiyo imeongeza pointi moja zaidi na kufanya tofauti kati yao na Yanga kuwa pointi mbili, huku wakiendelea kukaa kileleni.

Matokeo hayo yameifanya Mtibwa Sugar kushika nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 31 nyuma ya Yanga yenye pointi 43.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Willian anasema hakuna sababu ingemfanya kusalia Chelsea iwapo Antonio Conte angebakia

Willian alifunga magoli 13 na kutoa pasi 12za usaidizi katika mechi 55 za Chelsea msimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *