Home / Michezo / Yaya Toure asema Raheem Sterling angejiangusha

Yaya Toure asema Raheem Sterling angejiangusha

Refa Andre Marriner hakuona kosa upande wa Walker

Kiungo wa kati wa Manchester City Yaya Toure amesema winga wa klabu hiyo Raheem Sterling alifaa kujiangusha na kuishindia klabu yake penalti wakati wa mechi yao dhidi ya Tottenham Hotspur Jumamosi.

Mechi hiyo ilimalizika wka sare ya 2-2.

City walikuwa wanaongoza 2-1 pale Sterling alipopata mwanya wa kushambulia eneo la hatari.

Hata hivyo, alisukumwa na beki wa Spurs Kyle Walker ingawa hilo halikuonekana na mwamuzi wa mechi Andre Marriner.

Baada ya mechi, Walker alikiri “Sikuwa naenda kuufikia mpira.”

Toure amesema: “Ukiwa na uzoefu kama wangu, labda unaweza kujiangusha.”

Muda mfupi baada ya mfarakano kati ya Walker na Sterling, Tottenham walisawazisha kupitia Son Heung-min.

Sare hiyo iliwafanya City, ambao walikuwa wameongoza 2-0 wakati mmoja, kusalia nambari tano kwenye jedwali.

“Hizo ni alama mbili zinapotea,” Toure aliongeza.

“Tottenham ani wazuri. Wanacheza vyema sana, wana nguvu, wanapigania mipira, lakini tulistahiki alama hizo tatu.”

Kuhusu kisa cha Sterling, Toure alisema: “Alikuwa mkweli sana, anataka kutenda haki wakati wa mechi kama hizi. Iwapo kijana huyo ni mtu wa aina hiyo, huwezi kumwambia alikosa.

“Unapotazama, hangekosa kufunga – lakini Walker alimsukuma kutoka nyuma.

“Mwamuzi akitazama video baada ya mechi, atahisi haki haikutendeka. Sote hutenda makosa maishani, lakini hili ni chungu kulikubali.”

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Willian anasema hakuna sababu ingemfanya kusalia Chelsea iwapo Antonio Conte angebakia

Willian alifunga magoli 13 na kutoa pasi 12za usaidizi katika mechi 55 za Chelsea msimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *