Home / Habari Za Kitaifa / KIGAMBONI WATAFUTIWA SULUHU YA UMEME.

KIGAMBONI WATAFUTIWA SULUHU YA UMEME.

KUTOKANA na tatizo la umeme kukatika mara kwa mara na kwa vipindi virefu katika Wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) imewaomba wakazi wa wilaya hiyo kuwa wavumilivu wakati tatizo likitafutiwa ufumbuzi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Meneja wa Shirika hilo, Richard Swai, alisema shirika hilo linajitahidi kutatua tatizo hilo na kulimaliza kabisa.

“Tunawaomba wananchi kuwa na uvumivu tu kwa sababu tatizo hilo litakwisha, tumejipanga kukamilisha ujenzi wa vituo mbalimbali ikiwemo kipya ambacho kitajengwa Dege kata ya Somangila,” Alisema Swai.

Swai alisema umeme unaolisha Kigamboni unatoka Kipawa, hata hivyo njiani imelisha pia viwanda kadhaa na pia kituo cha kupooza umeme cha Chang’ombe.

“Laini hii imezidiwa na kutokana na urefu wake iko katika changamoto nyingi, tatizo likitokea popote kati ya Kipawa na Kigamboni laini huzimika na Kigamboni yote kukosa umeme,” alisema Swai.

Swai alisema mipango iliyopo ni ujenzi wa kituo cha kupooza umeme cha Mbagala cha 132/33kV ambacho kitalisha Toangoma, Mikwambe, Kibada na Kisarawe II, “kituo hiki tunatarajia June kiwe tayari,” alisema.

Aidha, alisema kuna ujenzi unaendelea wa kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Kurasini (132/33kV) ambapo njia nyingine italisha kata za Kigamboni ambazo ni Tungi, Vijibweni, Mjimwema, Somangila, Kimbiji hadi Pembamnazi.

Swai alisema Tanesco ina mpango pia wa kujenga kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha 132/33kV mtaa wa Dege kata ya Somangila ambapo tayari Tanesco imenunua eneo zaidi ya ekari 24 na tayari wameomba bajeti kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.

SOURCE HABARI LEO.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *