Home / Habari za Kimataifa / IRAN KULIPIZA KISASI DHIDI YA VIKWAZO VIPYA VYA MAREKANI.

IRAN KULIPIZA KISASI DHIDI YA VIKWAZO VIPYA VYA MAREKANI.

Iran iliwekewa vikwazo hivyo baada ya kufanya jaribio la kombora lake

Iran imeshutumu vikwazo vipya ilivyowekewa na Marekani na kuahidi kuchukua hatua za kulipiza kisasi.

Serikali ya Washington inasema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kufuatia jaribio la kombora lililofanywa Jumapili, ambalo Marekani imesema ni hatua ya Iran ya kuwasaidia magaidi katika shughuli zao mbovu duniani.

Wizara ya mashauri ya kigeni ya Iran ilisema kuwa vikwazo hivyo vinakiuka mkataba ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambap ulikubali kupunguza kasi ya kuimarisha shughuli zake za kinulikia.

waziri wa maswala ya kigeni nchini Iran Javad Zarif

Iran ilisema kuwa itawawekea watu fulani wanaoshukiwa kushirikiana na makundi ya kigaidi vikwazo na pia dhidi ya kampuni zingine za Marekani.

Marekani ilisema kuwa vikwazo vyake vitalenga kampuni 12 na watu 13 nchini Iran na kwingineko.

SOURCE BBC SWAHILI.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *