Home / Michezo / Christian Bassogog Mwanasoka Bora AFCON 2017.

Christian Bassogog Mwanasoka Bora AFCON 2017.

Christian Bassogog,Mchezaji bora wa kombe la Afrika,2017

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Cameroon, Christian Bassogog amechaguliwa kuwa Mwanasoka Bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika iliyomalizika nchini Gabon mwaka huu 2017.

Mchezaji huyo amekuwa msaada mkubwa kwa timu yake ya Cameroon kuweza kutwaa Kombe la AFCON, baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Misri kwenye mchezo wa fainali ambao ulipigwa katika dimba l’Amitie mjini Libreville na kutajwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashindano na Kamati ya Ufundi ya CAF na kikundi cha Watathmini.

Orodha ya waxchezaji wengine waliofanya vizuri katika michuano hiyo ni Mchezaji Bora wa Benjamin MOUKANDJO (Cameroon), Tuzo ya Fair Play – Misri, Mfungaji Bora-Junior KABANANGA (DRC) Mabao 3, Kikosi cha Mashindano cha CAF – Kipa Fabrice ONDOA (Cameroon),Mabeki- Modou Kara MBODJI (Senegal), Ahmed HEGAZY (Misri), Michael NGADEU (Cameroon)

Viungo-Charles KABORE (Burkina Faso), Daniel AMARTEY (Ghana), Bertrand TRAORE (Burkina Faso), Christian ATSU (Ghana), Mohamed SALAH (Misri) .

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Willian anasema hakuna sababu ingemfanya kusalia Chelsea iwapo Antonio Conte angebakia

Willian alifunga magoli 13 na kutoa pasi 12za usaidizi katika mechi 55 za Chelsea msimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *