Home / Michezo / Nchemba asema Singida itakuwa kama Leicester

Nchemba asema Singida itakuwa kama Leicester

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba amesema Singida United itakuwa kama Leicester City ya England ambayo ilipanda Ligi Kuu na kutwaa ubingwa kwa kuzibwaga timu kubwa.

Kauli ya Nchemba imekuja siku moja baada ya Singida United kukata tiketi ya kucheza Ligi Kuu kutoka kundi C katika ligi daraja la kwanza kwa kuifunga Alliance ya Mwanza mabao 2-0 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Namfua Singida juzi na kufikisha pointi 30 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote katika kundi hilo hata baada ya mechi za mwisho mwishoni mwa wiki hii.

Akizungumza juzi kwenye uwanja wa Namfua Singida baada ya mechi hiyo, Nchemba alisema: “Nimefurahi kama wana Singida wengine walivyofurahi kwani hili ni jambo ambalo lilisubiriwa kwa miaka mingi na mimi kama mdau wa mkoa wa Singida nitaendelea kuunga mkono timu yetu ili iweze kufanya vizuri zaidi kama Leicester City, inaenda kuchukua ubingwa,” alisema Nchemba.

Hata hivyo Leicester haikuendelea kufanya vizuri kwani baada ya kutwaa ubingwa msimu uliopita, msimu huu ipo kwenye ukanda wa kushuka daraja. Nchemba pia ni mdau mkubwa wa Yanga.

Naye kocha wa Singida United ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga, Fred Minziro alisema sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wa Singida wakiongozwa na mbunge Nchemba ndio sababu ya timu kupanda daraja.

“Ushirikiano wa wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, mbunge na mashabiki ambao wametuunga mkono kuhakikisha tunapata ushindi ndio siri kubwa ya ushindi wetu,” Minziro.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Willian anasema hakuna sababu ingemfanya kusalia Chelsea iwapo Antonio Conte angebakia

Willian alifunga magoli 13 na kutoa pasi 12za usaidizi katika mechi 55 za Chelsea msimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *