Home / Habari za Kimataifa / DONALD TRUMP AKUTANA NA BENJAMIN NETANYAHU.

DONALD TRUMP AKUTANA NA BENJAMIN NETANYAHU.

Rais Donald Trump wa Marekani akipeana mkono wa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wakati wa mkutano na waandishi habari, nchini Marekani

Rais Trump amemkaribisha waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika ikulu ya Marekani, na kusema atafanya kazi kwa bidii kwa kile alichokiita makubaliano ya amani kati ya Israel na Palestine.

Amesema pande zote mbili zitahitajika kuwa na maridhiamo, na kwamba angetaka Israel isitishe kidogo ujenzi wa makazi unaoendelea.

Kwa upande wake, bwana Netanyahu amesema Israel sharti ihakikishe kuwepo kwa usalama katika eneo la linalokaliwa la West Bank.

Amesema hivi sasa kuna fursa kubwa ya kuwepo kwa makubaliano ya amani kwa kushirika wajumbe wengine wa nchi za kiarabu.

Bwana Netanyahu pia amesema anaamini kwamba uongozi wa bwana Trump unatoa fursa ya kihistoria ya kubadilisha kile alichokiita kama kuwepo kwa wimbi la waislamu wenye msimamo mkali.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *