Home / Habari Za Kitaifa / MTAKA ASIFIWA KWA KUONA MBALI.

MTAKA ASIFIWA KWA KUONA MBALI.

MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, ameitwa twiga wa mkoa kutokana na uwezo wake wa kuona mbali na kufikiria haraka katika kuhakikisha analeta mabadiliko chanya katika mkoa wake.

Akizungumza katika Jukwaa la Biashara lililoandaliwa na kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Mbunge wa Busega, Dk Raphael Chegeni, alimpongeza Mtaka akisema anashukuru mkoa huo kupata mkuu wa mkoa mwenye uwezo kama yeye.

“Ndugu zangu, Waswahili wanasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Mkuu wetu wa mkoa anafanya mambo mazuri na makubwa sana kwa faida ya mkoa wetu.”

Baada ya kusema hayo, Chegeni aliyekuwa ameketi meza kuu akamgeukia Mtaka.

“Ndugu mkuu wa mkoa, hakika wewe ni twiga wetu. Unaona mbali kwa ajili ya mkoa wetu.”

Akiteta na HabariLeo nje ya ukumbi kulikokuwa kunafanyika Jukwaa hilo, Mbunge wa Itilima ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani humo, Njalu Silanga, alisema wanashukuru kuwa na mkuu wa mkoa anayeona fursa nyingi katika mkoa huo na kutaka kuona zinawanufaisha wana Simiyu na kwamba wana imani kuwa atasaidia sana kuupaisha mkoa wao kiuchumi.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *