Home / Michezo / Manchester United, AS Roma zashinda Europa Ligi

Manchester United, AS Roma zashinda Europa Ligi

Manchester United katika furaha ya bao 3-0

Mashetani wekundu wa Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Saint-Etienne, mabao yote ya United yamefungwa na Zlatan Ibrahimovic.

As Roma wakicheza ugenini wameshinda kwa mabao 4-0 dhidi ya Villarrea, Tottenham Hotspurn wamepoteza mchezo ugenini kwa kuchapwa kwa bao 1-0 na Kaa Gent.

AZ Alkmaar wamelala nyumbani kwa kufunga 4-1 na Lyon, wajerumani wa Borussia Moenchengladbach nao wamepoteza kwa Fiorentina kwa kufungwa bao 1-0.

Athletic Bilbao wameshinda nyumbani kwa 3 – 2 dhidi ya Apoel Nicosia, Celta Vigo wamechapwa na Shakhtar Donetsk kwa bao 1-0. Anderlecht wameshinda 2 – 0 dhidi ya Zenit St. Petersburg.

Paok Thessaloniki wameshindwa kutamba nyumbani kwa kufunga na Schalke kwa 3-0,

Matokeo mengine

  • Astra Giurgiu 2 – 2 Genk
  • Rostov 4 – 0 Sparta Prague
  • Ludogorets Razgrad 1 – 2 FC Koebenhavn
  • Olympiacos 0 – 0 Osmanlispor FK
  • Hapoel Beer Sheva 1 – 3 Besiktas
  • Legia Warszawa 0 – 0 Ajax

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Man United iko mbioni kumtangaza Mkurugenzi wa michezo

Golikipa wa zamanI wa Man United Edwin Van De Sar anatajwa kuwa na nafasi kubwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *