Home / Habari Za Kitaifa / DC Hapi avalia njuga uvuvi haramu

DC Hapi avalia njuga uvuvi haramu

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi ametangaza vita dhidi ya uvuvi haramu, huku akikabidhi majina ya watu 21 yakiwemo ya viongozi wanaojihusisha na uvuvi huo kwa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni.

Aisha, Mkuu huyo wa wilaya amesimamia uteketezwaji wa zana haramu za uvuvi za thamani ya Sh milioni 60 ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa vita dhidi ya uvuvi haramu.

Hapi alitangaza vita hiyo jana akiwa katika ziara ya siku 10 ya awamu ya pili ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya yake ambapo alisema, uvuvi huo unahatarisha uwepo wa samaki kutokana na kutumia zana zinazoangamiza mazalia ya samaki.

Alisema wavuvi haramu wamekuwa wakivua samaki ambao hawastahili kuvuliwa na kwamba wapo baadhi ya watu wanaotumia mabomu na milipuko wanaoenda chini ya bahari na kulipua.

“Wavuvi haramu wanatumia mabomu na milipuko, wanaua mazalia ya samaki, kama tusipochukua hatua mapema, watoto na vizazi vyetu hawatakula samaki,” alisema Hapi.

Hapi alisema amekabidhi majina hayo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda ili kuyafanyia uchunguzi na ikiwa watabainika kuhusika na uvuvi huo ili wachukuliwe hatua kali za listeria.

Alisema watu wanahusika katika uvuvi haramu wana nguvu kubwa lakini Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kutokomeza uvuvi haramu.

“Hatuwezi kuvumilia hali hii kuendelea, mbali na kimaliza mazalia ya samaki lakini hata wale watalii wanaokuja kuzamia kuangalia mandhari hawatakuja,” alisema.

Hapi alisema wavuvi hao haramu wamekuwa wakitumia milipuko ambayo ni hatari na endapo isipozuiliwa inaweza ikachangia kujitokeza kwa matukio ya kihalifu pamoja na ugaidi.

Aliongeza kuwa utumiaji wa zana hizo haramu una madhara mengi ikiwemo watu kupata ulemavu wa viungo vya mwili na wengine kupoteza maisha kutokana na milipuko ya mabomu.

Aliongeza kuwa kila siku milipuko 50 imekuwa ikisikika kila siku katika ukanda wa fukwe za manispaa hiyo.

Ofisa Uvuvi Wilaya ya Kinondoni, Grace Katama alisema vifaa hivyo asilimia 80 vimekamatwa maeneo ya Kawe na Kunduchi.

Alisema shughuli za ukamataji zilianza Septemba mwaka jana hadi sasa na kwamba Matukio ya milipuko yamekuwa mengi

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *