Home / Habari za Kimataifa / Uganda yazindua mpango kusaidia wanawake tasa

Uganda yazindua mpango kusaidia wanawake tasa

Wanawake wengi hukabiliwa na unyanyapaa wasiopopata watoto

Uganda imezindua mpango wa kuwasaidia wanawake wagumba kukabiliana na unyanyapaa.

Wanawake wengi wasioweza kupata watoto wanasema wanapitia mengi yakiwemo waumezao kuwafukuza kutoka majumbani mwao kwa sababu ya ugumba.

Mwandishi wetu wa Kampala Siraj Kalyango anasema inakadiriwa kuwa nchini Uganda kuna wanawake wagumba takriban millioni tano, kwa mujibu wa waziri wa taifa wa afya Bi Sarah Opendi.

Kawaida wanawake hawa hulaumiwa kwa tatizo hilo sugu japo waziri anasema huenda shida iko kwingine.

Bi Opendi anasema kuwa tatizo hili linaathiri wanawake kati ya asilimia 10 na 15, na kuongeza kuwa uchunguzi uliofanywa unamatokeo ya kusisimua.

Waziri ametoa kauli hiyo wakati wa kuzindua mpango utakao wasaidia wagumba wa Uganda kujitosheleza kimaisha baada ya kunyanyashwa.

“Uzinduzi wa mpango huu utakuwa na manufaa mengi kama anavyofafanua,” anasema mmoja wa wanawake waliohudhuria.

Waziri amesisitiza kuwa wanawake wengi hawajui kuwa shida ya kutozaa sana sana ni ya wanaume na hivyo baadaye wengi wakifahamu hilo hawatakubali kunyanyaswa na kufukuzwa kutoka nyumbani kwao eti kwa sababu wameshindwa kuzaa.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *