Home / Habari za Kimataifa / Panya asababisha safari ya ndege kuchelewa Uingereza

Panya asababisha safari ya ndege kuchelewa Uingereza

Panya asababisha safari ya ndege kuchelewa Uingereza

Safari ya ndege kutoka uwanja wa Heathrow hadi San Francisco, ilichelewa kwa saa kadhaa baada ya panya kuonekana ndani ya ndege.

Abiria waliokuwa wakisafiri kwa ndege hiyo ya shirika la Uingereza, walikuwa tayari wameingia ndani ya ndege hiyo wakati lilitolewa tangazo kuwa ingechelewa.

Carly, ambaye alikuwa ndani ya ndege, alisema kuwa mhudumu alitangaza, “walisema kitu kisicho cha kwaida kimetokea”

Panya

Kisha mhudumu huyo akasema wameambiwa ndege nyingine imepatikana lakini abiria wangesubiri saa kadhaa ili kuanza safari.

Kisha safari nyingine ikaanza saa nne baadaye.

Shirika la ndege la Uingereza lilisema; “Tunaelewa kuwa karibu kila mtu anataka kusafiri nasi hadi San Francisco, lakini wakati huu kulikuwa na mteja mdogo ambaye lazima tungemtoa.

“Kila mmoja aliye na miguu miwili kwa sasa yuko safarini kuenda California, na tunaomba radhi kwa kuchelewa.”

Panya asababisha safari ya ndege kuchelewa Uingereza

source bbc swahili

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *