Home / Habari za Kimataifa / Mshauri wa Trump alitaka Fethullah Gulen kuondolewa Marekani

Mshauri wa Trump alitaka Fethullah Gulen kuondolewa Marekani

Aliyekuwa mshauri wa maswala ya kiusalama wa rais wa Marekani Donald Trump, Michael Flynn

Aliyekuwa mshauri wa maswala ya kiusalama wa rais wa Marekani Donald Trump ,Michael Flynn alizungumza kuhusu kumuondoa kiongozi wa dini aliye mafichoni Marekani anayesakwa na Uturuki kulingana na aliyekuwa mkurugenzi wa idara ya ujajusi James Woolsey.

Uturuki inamshtumu kiongozi huyo wa dini Fethullah Gulen kwa kuandaa mapenduzi ya mwaka uliopita nchini Uturuki.

Katika mahojiano yalirekodiwa katika kanda ya video Bwana Woolsey aliambia jarida la Street Jaournal alikuwa katika mazungumzo kuhusu njia za kumuondoa kiongozi mbali na hatua halali za kisheria.

Hatahivyo Bwana Flynn amekana madai hayo ya Whoolsey.

Mkutano huo ulifanyika mnamo mwezi Septemba katika hoteli moja mjini New York.

Wale waliohudhuria mazungumzo hayo ni pamoja Flynn wakati huo akiwa mshauri wa bwana kampeni ya bwana Trump kuhusu maswala ya kiusalama, mwana wa kambo wa rais wa Uturuki Tayyip Erdogan pamoja na waziri wa maswala ya kigeni nchini Uturuki Mevlut Cavusoglu kulingana na jarida la Wall Street Journal.

Uturuki inamshtumu kiongozi wa dini Fethullah Gulen kwa kuandaa mapenduzi ya mwaka uliopita nchini Uturuk

Bwana Woolsey ambaye pia alikuwa mashauri wa kundi la kampeni la Trump alikiri kwamba alichukua tahadhari kwa sababu aliwasili kuchelewa katika mkutano huo.

Lakini aliambia jarida hilo kwamba kuliwa na mazungumzo mazito kuhusu kutafuta njia za kumfurusha bwana Gulen kutoka Marekani na kumpeleka Uturuki.

”Unaweza kusema ulikuwa mkutano wa kutafuta mbinu, lakini ulikuwa unaangazia swala zito ambalo lilikuwa linakiuka sheria”.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *