Makala

Ubora Wa Elimu

Uislamu unahimiza Elimu kutokana Umuhimu wake na Ubora wake Ukirejea katika uteremshwaji wa Wahyi kwa Mtume Muhammad (S.A.W)Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani unakuja kukuta kwamba Aya za Mwanzo 5 Kumteremkia Mtume zilikuwa zinazungumzia Elimu (Kusoma).

M/Mungu anasema ” Soma kwa Jina la Mola wako ambaye ameumbaa …”. Qur an.
Elimu ndio pambo zuri , lenye Thamani kuliko Mapambo yote anayojipamba nayo Mwanadamu.

Elimu ndio mwangaza na taa pekee inayomuangazia mwanadamu katika Maisha ya ulimwengu huu.

Elimu ndio chombo pekee anachoweza kukitumia mwanadamu katika kumtii Mola wake, kwani kutokana na elimu ndipo mwanadamu huweza kujua halali na haramu na akapambanua baina ya lenye kunufaisha na lenye kudhuru.

Elimu ndio njia pekee ambayo inaweza ikakutoa au kulitoa Taifa katika Kiza cha Utororo na kuwa katika Mwanga wa Maendeleo na Utukufu wa Elimu ndio Mataifa Mengi yamesonga mbele.
Isipokuwa tutambue kwamba Elimu pekee bila ya Vitendo haina faida wala Msaada kwa Msomaji SUBHANA ALLAH .

Ili Elimu iwe Elimu chukua Muongozo wa Wanachuoni huu (Elimu bila ya matendo ni kama mti usiotoa matunda).

UKIREJEA AYA TULIYO ANZA NAYO ” Soma kwa Jina la Mola wako ambaye ameumbaa …”.
Tuzisafishe Nyoyo zetu ki Nia katika Usomaji wetu uwe kwa Ajili ya M/Mungu na wala si kutaka kujulikana kwamba wewe ni Msomi .

Pili chukua Muongozo huu Mwenye kutaka kupata elimu ya nyingi , pamoja na kufanya juhudi ya kusoma basi ajilazimishe sana kumcha Mwenyezi Mungu katika Dhahiri na Siri SUBHANA ALLAH , M/MUNGU : “NA MCHENI MWENYEZI MUNGU NA MWENYEZI MUNGU ATAKUELIMISHENI; NA MWENYEZI MUNGU NI MJUZI WA KILA KITU” Qur an Sura 2 Aya 282.

Katika kuonyesha ubora na utukufu wa elimu Mwenyezi Mungu anatuambia: “SEMA, JE WANAWEZA KUWA SAWA WALE WANAOJUA NA WALE WASIOJUA?..” Qur an Sura ya 39 Aya 09.
Jibu la hawawezi kuwa sawa wenye kujua na wasio Jua ….
SOMA HADITHI YA BWANA MTUME MUHAMMAD ( S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani ” Kutafuta elimu ni faradhi ya lazima kwa kila muislamu (Neno Muislamu linakusanya Mwanamume na Mwanamke)”. kama alivyosema Mtume.

FAIDA ZA KUSOMA.
Ziko faida nyingi sana ambazo anazipata Mtu mwenye kusoma miongoni Mwazo tumekwisha tangulia zitaja.

ila kubwa katika nyengine faida za kusoma ni kukupa wewe Msomi Muongozo wa kuweza kutekeleza vyema kazi ya kulingania kama M/MUNGU ANAVYOSEMA “WAITE(watu) KATIKA NJIA YA MOLA WAKO KWA HIKIMA NA MAWAIDHA MEMA NA UJADILIANE NAO KWA NAMNA ILIYO BORA… “Qur an Sura ya 16 Aya 125.

Vilevile M/Mungu anasema “MWENYEZI MUNGU ATAWAINUA WALE WALIOAMINI MIONGONI MWENU; NA WALIOPEWA ELIMU WATAPATA DARAJA ZAIDI” Qur an Sura ya 58 Aya 11. Hii nayo ni moja katika faida za Msomi.

Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close