Makala

ADABU ZINAZOTAKIWA KUFUATWA KATIKA SIKU YA EID.

1.Muislamu anatakiwa katika siku za Eid akoge (Josho kubwa) , ajitie manukato (mwanamume) na avae nguo nzuri za kupendeza.

Ni sunna kula kwanza kabla ya kwenda kuswali swala ya Eidil-Fitri kinyume na Eid -Adh-haa unatakiwa ule ukitoka kuswali kama alivyo tuelekeza Mtume.

2.Kuleta Takbira kwa wingi tangu usiku wa Eid zote mbili.

MUDA WA TAKBIRA KWA EID – EL FITRI zinaanza Usiku wa Eid na kuendelea Mpaka baada ya swala tu, ama zile za Eid l Adh-haa hudumu mpaka siku ya mwisho ya kuanikwa Nyama (Alasiri ya mwezi 13 – Mfunguo tatu).

MATAMSHI YA TAKBIRA ZA EID.

ALLAAHU AKBAR ALLAAHU AKBAR ALLAAHU AKBAR . LAA ILAAHA ILLAL-LAAH WALLAAHU AKBAR . ALLAAHU AKBAR WALILLAAHIL-HAMDU. ALLAAHU AKBAR KABIYRAA . WAL-HAMDU LILLAHI KATHIYRAA. WASUB-HAANALLAAHI BUKRATAN WA ASWIYLAA. LAA ILAAHA ILLAL-LAAHU WAHDAU. SWADAQA WA’ADAU. WANASWARA ‘ ABDAU . WA A’AZZA JUNDAU WAHAZAMAL – AHZAABU WAHDAU. LAA ILAAHA ILLAL-LAAHU. WALAA NA-‘BUDU ILLAA IYYAAU MUKHLISWIYNA LAHUD – DIYN WALAU KARIHAL- KAAFIRUUN.

ALLAAHUMMA SWALLI ALAA SAYYIDNAA MUHAMMAD WA ALAA AALI SAYYIDNAA MUHAMMAD . WA ALAA ASW-HAA BI SAYYIDNAA MUHAMMAD WA ALAA ANSWAARI SAYYIDNAA MUHAMMAD WA ALAA DHURRIYATI SAYYDINAA MUHAMMAD . WASALLIM TASLIYMAN KATHIRYRAA.

3.Ni suna kwenda msikitini kwa njia moja na kurudi kwa njia nyingine isiyokuwa ile uliyo tumia wakati wa kwenda.

4.Vilevile ni sunna waislamu kupeana mikono siku ya Eid , na kuombeana Dua kwa Kusema ( TAQABBALALAAHU MINNAA WA MINKA ) (Mwenyezi Mungu atutakabalie Ibada zetu Sisi na wewe). Hii Ni Dua Itikia Amiin.

Hivi ndivyo ilivyopokelewa Maswahaba wa Mtume walikuwa wanapokutana siku ya Eid huambiana (huombeana) ” Taqabbalal-laahu Minnaa waminkum ” Na si kama Mazoea yetu ikiwa kama Mazoea yatakuja baada ya kuombeana Dua kwa Namna tuliyo elekeza hakuna tatizo Mazoea yetu ” MKONO WA EID UKINIONA KIMNYA UJUE SINA “.

5.Eid ni siku ya Furaha hivyo basi furahi na wafurahishe familia yako kwa Vyakula , Vinywaji ( Vinywaji vya halali) pasina kufanya fujo (Israafu) na hapa ni muhimu tuwakumbuke Ndugu zetu wasio na uwezo kwa sadaka ili nao wapate furahi siku hii tukufu.

Siku ya Eid ni Siku ya Kula na Kunywa ( Vinywaji vya halali) , Kumshukuru M/Mungu , kutembelea Ndugu , Jamaa na Marafiki na Mengi ya kheri yaliyo katika ratiba zako.

TAMBUA Siku hii hairuhusiwi kufunga kwa Mtu yeyote .

Baada ya kusherehea Siku ya Eid inayo fata Ni Sunna iliyokokotezwa na Mtume nayo ni Sunna ya Funga ya Sita .

Ni Bora kufunga Siku ya Pili au Mwezi Pili Shawali lakini inaruhusiwa kufunga Muda wowote Funga hii ya Sita isipokuwa Isitoke tu ndani ya Mwezi wa Shawali

Imepokewa hadithi na Abu Ayoub (Radhi za M/Mungu zimshukie Juu yake ) kwamba Mtume Muhammad (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie juu yake na amani amesema, ” Atakayeufunga mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani, na kisha akaufuatishia Mwezi huo wa Mtukufu wa Ramadhani na siku sita za Mwezi wa Shawali(Mfungo mosi) itakuwa kama kufunga mwaka mzima” kama alivyosema Mtume hadithi imepokelewa na Imamu Muslim.

Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close