Home / Michezo / Rekodi tamu wachezaji Taifa Stars

Rekodi tamu wachezaji Taifa Stars

Baada ya mechi mbili za kimataifa zilizochezwa na timu ya taifa Taifa Stars, baadhi ya wachezaji wameweka rekodi mbalimbali wakiwa na timu hiyo.

Jumamosi iliyopita, Stars ilicheza dhidi ya Botswana na kushinda mabao 2-0, yaliyofungwa na kapteni wa timu hiyo, Mbwana Samatta.

Siku ya Jumanne ilicheza tena mechi ya pili, pia ikitambuliwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) dhidi ya Burundi.

Katika mechi hiyo, Stars ilishinda mabao 2-1, yaliyofungwa na Simon Msuva na Mbaraka Yusuph.

Hawa ni baadhi ya wachezaji walioweka rekodi baada ya mechi hizo mbili za kirafiki.

  1. Mbwana Samatta

Ameweka rekodi ya kufunga magoli mawili kwenye mechi moja ya timu ya taifa, Taifa Stars.

Hakuwahi kufanya hivyo mwanzo. Mabao hayo yamemfanya straika huyo anayeichezea KRC Genk ya Ubelgiji kutimiza idadi ya mabao 13 katika mechi 38 alizochezea nchi yake

Kati ya mabao hayo 13, bao moja alilifunga katika mechi ya Chad ambayo hata hivyo matokeo yake yalifutwa kufuatia nchi hio kujiondoa mashindanoni kwa kile walichodai kukumbwa na ukata.

Anakuwa mchezaji wa pili kufunga magoli mengi kwenye timu ya taifa kwa miaka ya hivi karibuni

Anayeongoza kufunga magoli mengi mpaka sasa kwenye timu ya taifa kwa miaka ya karibuni ni Mrisho Ngasa ambaye ameifungia Stars jumla ya magoli 25.

  1. Himid Mao

Kiungo huyu wa kukaba wa Taifa Stars, baada ya mechi hizo mbili ameweka rekodi ya mechi zote mfululizo wa timu hiyo, tangu mwaka 2015.

Himid hajawahi kukosa mechi yoyote ya timu ya taifa na mpaka sasa ameshafikisha jumla ya michezo 12.

Mchezaji huyo anayetokea Azam FC, ambaye pia ni nahonda msaidizi wa Stars, alianza kuichezea timu hiyo katika mechi za kuwania kufuzu

Fainali za Kombe la Mataifa Afrika AFCON zilizofanyika mwanzoni mwa mwaka huu nchini Gabon. Hakuwahi kuitwa chini ya kocha Mart Nooij lakini mara tu Boniface Mkwasa alipochukua usukani alimjumuisha katika kikosi na kumuanzisha katika pambano dhidi ya Nigeria lililopigwa mwaka Septemba 5, 2015 jijini Dar.

Ingawa pia aliicheza mechi za Kombe la Chalenji nchini Ethiopia mwaka 2015 lakini hazikujumuishwa kwenye rekodi hii kwa kuwa kikosi hicho kinajulikana kama Kilimanjaro Stars kilichohusu wachezaji kutoka Tanzania Bara tu.

  1. Mbaraka Yusuph

Straika kinda wa Kagera Sugar, ameweka rekodi ya kufunga goli kwa mara ya kwanza akiwa kwenye kikosi cha Taifa Stars.

Mchezaji huyo alichaguliwa kwa mara ya kwanza na kocha Salum Mayanga, amefunga goli kwenye mechi ya kwanza tu aliyocheza, tena akitokea

benchi.

Ni goli la pili alilolifunga dhidi ya Burundi ya kuipa ushindi Taifa

Stars wa mabao 2-1.

  1. Mzamiru Yassin

Ni kiungo ambaye ameweka rekodi ya kuitwa kwenye timu hiyo kwa mara ya kwanza na kuichezea timu hiyo mechi zote mbili.

Mzamiru anayeichezea timu ya Simba, ni mmoja kati ya wachezaji wachache ambao wamechaguliwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi chaTaifa Stars.

Wengi ni wale ambao wamekuwa wakichaguliwa mfululizo, au walishawahi kuchaguliwa huko nyuma na wamerudishwa.

Lakini kiungo huyo aliingia kipindi cha pili kwenye mechi dhidi ya Botswana na pia alianza dhidi ya Burundi, lakini baadaye alitoka kipindi cha pili.

Kwenye mechi zote hizo alicheza kwa kiwango cha hali ya juu, akitawala sehemu ya kiungo na kuwa sehemu ya ushindi wa timu hiyo.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *