Home / Habari za Kimataifa / Taiwan kuunda manowari zake kujilinda dhidi ya Uchina

Taiwan kuunda manowari zake kujilinda dhidi ya Uchina

Taiwan kuunda manowari zake kujilinda dhidi ya Uchina

Taiwan imethibitisha kuwa, ina nia ya kuunda jumla ya manowari nane ya kivita, ili kujilinda dhidi ya uchokozi wa China.

Ni mara ya kwanza kwa taifa hilo kutengeneza vyombo hivyo vya majini.

Mara nyingi imekuwa ikitegemea kununua zana za kivita kutoka kwa Marekani, lakini hayo yamepungua pakubwa katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na hatua ya China ku-i-zuia isifanye hivyo, huku ikitaka kisiwa hicho kujiunga tena na kuwa chini ya utawala wake.

Kwa sasa Taiwan, ina manowari nne tu ambazo ni nzee- ambapo mawili kati yao yalinunuliwa kutoka Uholanzi na mbili kutoka Marekani.

Vyombo hivyo viwili vya Marekani, viliundwa wakati wa vita kuu vya pili duniani.

China na Marekani wamelaumiwa kwa kuweka silaha kusini mwa bahari ya China ambapo China inang’ang’ania eneo hilo pamoja na Vietnam, Ufilipino, Taiwan, Malaysia na Brunei

Marekani inasema kuwa kwa mujibu wa sheria yake, ina wajibu wa kuisaidia Taiwan kujilinda.

Rais Trump ametabiri kuwa mazungumzo ya Alhamisi na rais wa China Xi Jinping yatakuwa magumu.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *