Makala

Ziwa Ngozi, kivutio cha utalii Nyanda za Juu Kusini

ZIWA Ngozi ni la pili kwa ukubwa katika maziwa yaliyotokana na volkano barani Afrika. Ziwa hili linapatikana karibu na Tukuyu, mji mdogo wa Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Ziwa hili linalovutia watalii wengi kwa sasa liko umbali wa kilomita 38 tu kutoka Mbeya mjini.

Ni sehemu ya mgongo wa safu wa mlima Uporoto, likiwa umbali wa mita 2,620 kutoka usawa wa bahari. Liko kwenye msitu mnene wa Uporoto ambao ni hifadhi ya akiba yenye ukubwa wa hekta 9,332. Halikadhalika ni rahisi kupanda juu ya mlima wa volkano na kujionea ziwa kwa ndani. Kwa mujibu wa wataalamu wa mwangwi, sakafu yake ni bapa na hakuna matuta.

Ziwa Ngozi halikabiliwi na mabadiliko ya kupanda na kushuka kwa maji na kunakuwa na tofauti ndogo wakati misimu ya ukame na mvua. Joto la juu la ziwa hili ni nyuzi joto 18 ikiwa ni tofauti ndogo tu ya msimu. Kina cha maji cha Ziwa hilo hujaa hadi kufikia kilomita 2.5 na lina upana wa kilomita 1.6 hivyo kufanya kuwa ziwa la pili barani Afrika lililotokana na shimo lililoachwa na mlipuko wa volkano.

Hekaya zinasema kuwa misitu unaozunguka ziwa hilo unatawaliwa na watu wa kabila la Wasafwa ambao kiasili walikuwa ni wawindaji. Huu ni mlima iliotokana na mlipuko wa mara moja wa volkano, ingawa taarifa za kina hajathibitishwa na kuwekwa wazi. Ziwa hilo lina samaki na maji yake ya kina na yanaonekana na rangi ya kijani. Wenyeji kutumia njia yenye mwinuko sana kwenda chini kwenye pwani ya ziwa hilo kuvua samaki.

Simulizi za sasa kutoka kwa wananchi wa eneo hilo, zinaonesha uwepo wa imani kwamba kuna nyoka mwenye vichwa kumi na mbili anayelinda hazina za Ujerumani zinazodaiwa kutunzwa au kufukiwa katika ziwa hilo. Kivutio kubwa katika ziwa hilo ni pamoja na kutembea umbali wa takribani saaa mbili kutoka gari linapoishia kuelekea juu ya mlima wa volkano ili kuweza kuona mandhari nzuri ya ziwa hilo.

Alama ya safari ya kufika Ziwa Ngozi inaanzia katika msitu wa kijani uliostawi sawia, wenye migomba ya ndizi pori na mianzi iliyoshamiri na mikubwa. Njia ya kufikia kwenye mgongo wa mlima Uporoto ili kuona vizuri mandhari ya ziwa hilo, maeneo mengine ni nyembamba mno kiasi cha kuhitaji umakini zaidi katika kupita. Mambo mengine ya kufurahisha katika safari ya kufikia Ziwa Ngozi ni uwepo wa kima punju wenye rangi nyeusi na nyeupe na eneo ambalo linanyesha mvua kila wakati.

Pia kuna aina kadhaa ya ndege ambao hutoa sauti mbalimbali za kuvutia ndani ya msitu huo mara kwa mara. Katika msitu huo pia ni maarufu kwa kuwa na vinyonga wa aina mbalimbali. Kwa ujumla ugumu wa kupanda kilele cha mgongo wa mlima Uporoto ni wa wastani na mtu hutumia muda mfupi kuweza kufika katika eneo ambalo ni rahisi kuona mandhari nzima ya Ziwa Ngozi. Ni mwendo wa saa moja hadi saa moja na nusu.

Lakini pia kuna maeneo ambayo yanahitaji watu kushikana mikono ili kupita na pindi unapofika kwenye kilele cha mlima huo unaweza kupata hewa mwanana na ya asili huku ukiona mandhari ya ziwa lililotokana na shimo la volkano ambalo limezungukwa na kingo zenye msitu. Ukibahatika kufika kwenye ziwa hilo unakutana na hali nzuri isiyo na ukungu. Unaweza kujionea mandhari nzuri hali ya rangi ya maji.

Ni vyema ukipata nafasi ukatumia fursa yako, kwenda kujionea vivutio vya utalii katika Nyanda za Juu Kusini ikiwa ni pamoja na Ziwa Ngozi, ambalo ni ziwa la pili kwa ukubwa barani Afrika lililotokana na shimo la volkano.

Makala haya yamepatikana kwa msaada wa mtandao wa intaneti.

Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close