Home / Habari Za Kitaifa / Polisi bado wamshikilia Msambatavangu

Polisi bado wamshikilia Msambatavangu

JESHI la Polisi mkoani Iringa linaendelea kumshikilia Mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Dk Jesca Msambatavangu anayetuhumiwa kumshambulia na kumsababishia maumivu makali mwilini mwanamke mmoja, ambaye jina lake halijafahamika.

Mpaka jana jioni, wakili wake aliyetajwa kwa jina moja la Chaula na wadhamini wake, walikuwa wakiendelea na taratibu za kumdhamini kada huyo wa CCM wa zamani huku kukiwa hakunataarifa zozote zinazoashiria kupewa dhamana hiyo.

Akizungumza kwa kifupi kuhusu tukio hilo juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi alisema kada huyo wa zamani wa CCM alikamatwa juzi mchana, akituhumiwa kutenda kosa hilo wiki iliyopita akiwa na wenzake ambao majina yao yamehifadhiwa, kwa kuwa wanaendelea kutafutwa.

Mjengi alisema Dk Msambatavangu na wenzake, wanadaiwa kumshambulia mwanamke mmoja mkazi wa Kibwabwa (hakutajwa jina kwa sababu za kiupelelezi).

source habari leo

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *