Home / Habari za Kimataifa / Mwanajeshi ajipiga picha akiuawa Afghanistan

Mwanajeshi ajipiga picha akiuawa Afghanistan

Picha iliopigwa na mwanajeshi huyo wakati alipokuwa akifanya zoezi la kijeshi nchini Afghanistan

Picha moja iliochukuliwa na mpiga picha wa jeshi nchini Marekani wakati yeye na wanajeshi wengine wanne waliuawa katika mlipuko imetolewa na jeshi la Marekani.

Mwanajeshi Hilda Clayton mwenye umri wa miaka 22 na wanajeshi wanne wa Afghanistan waliuawa wakati bomu lilipolipuka wakati wa zoezi la kijeshi mnamo tarehe 2 mwezi Juali 2013.

Picha hii ilichukuliwa na mwanajeshi mwengine ambaye alikuwa akijifunza na Clayton

Jeshi la Marekani pia lilitoa picha ya mwanajeshi wa kike wa Afghanistan ambaye mtaalam Clayton alikuwa akijifunza naye kupiga picha .

Pia alifariki.

Kifo cha Clayton ni ishara kwamba wanajeshi wa kike wanazidi kukabiliwa na hatari wakati wa mafunzo pamoja na vita na wenzao wa kiume.

Clayton alikuwa mkaazi wa jimbo la Georgia nchini Marekani

Ajali hiyo ilitokea katika mkoa wa mashariki wa Laghman.

Jarida la jeshi lilichapisha picha hizo.

Mwanajeshi katika shindano la Hilda Clayton kuwania mpiga picha bora

 

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *