Home / Habari za Kimataifa / Trump ailaumu China wa kufanya biashara na Korea Kaskazini

Trump ailaumu China wa kufanya biashara na Korea Kaskazini

Marekani na Korea Kusini walifyatua makombora ya masafa marefu kuenda bahari ya Japan

Rais wa Marekani ameishutumu China kufuatia hatua ya Korea Kaskazini kulifanyia majaribio kombora la masafa marefu, na kuilaumu kwa kuendelea kufanya biashara na Korea Kaskazini.

Marekani na Korea Kusini zilifanya majaribio ya makombora ya masafa marefu katika bahari ya Japan kujibu hatua hiyo ya Korea Kaskazini.

China na Urusi wamezitaka pande hizo kuacha kuonyesha ubabe wao wa kijeshi na kusema wanapinga majaribio yoyote ya kubadilisha uongozi nchini Korea Kaskazini.

Jaribio la kombora ambalo ni la hivi pudne kati ya majaribio kadha, lilienda kinyume na marufuku ya baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa.

Kombora la ICBM lililofyatuliwa na Korea Kaskazini

Marekani imetaka kufanyika mkutano wa dharura na baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa kujadili suala hilo.

Trump alifanya mazungumzo na Rais wa China Xi Jinping katika makao yake ya kifahari huko Florida mwezi Aprili.

Korea Kaskazini: Kombora letu linaweza kufika Marekani

Trump alisifu hatua alizopiga na China baada ya mkutano huo.

Takwimu zinaonyesha kuongezeka kwa biashara kati ya China na Korea Kaskazini.

Rais Trump sasa aneelekea nchini Poland na Ujerumani ambapo atakutana na Bwana Xi kwa mara ya pili.

Rais Trump sasa aneelekea nchini Poland na Ujerumani ambapo atakutana na Bwana Xi kwa mara ya pili.

China ambaye ni mshirika mkubwa wa kiuchumi wa Korea Kaskazinia na Urusi, imetaka Korea Kaskazini kuachana na progamu yake ya makombora ya masara marefu.

Bwana Xi na rais wa Urusi Vladimir Putin waliokutana mjni Moscow siku ya Jumanne walisema pande hizo zinastahili kuanza mazungumzo.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *