Home / Habari za Kimataifa / Watu wanne wauawa na washukiwa wa al-Shabab Lamu, Kenya

Watu wanne wauawa na washukiwa wa al-Shabab Lamu, Kenya

Watu wanne wameuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa al-Shabab katika eneo la Hindi katika kaunti ya Lamu katika eneo la pwani nchini Kenya.
Kamishna wa kaunti hiyo Gilbert Kitiyo ameambia BBC kwamba maafisa wakuu wa usalama katika kaunti hiyo wanakutana na watatoa maelezo zaidi baada ya mkutano huo.
Gazeti la kibinafsi la Standard linasema wakazi wamejitokeza barabarani katika mji huo kuandama kulalamikia ‘kukawia’ kwa maafisa wa usalama kufika eneo la shambulio.
Kenya yaanza kuangusha mabomu ‘msitu wa al-Shabab’
Kisa hicho kimetokea siku chache baada ya watu watatu kuuawa wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la al-Shabab waliposhambulia basin a gari eneo la Nyongoro, Witu katika kaunti hiyo ya Lamu.
Gazeti la Standard linasema visa vya mashambulio vimeongezeka eneo hilo wiki za hivi karibuni.
Kamishna wa kanda ya Pwani Nelson Marwa majuzi alitangaza kwamba maafisa wa usalama wangeanza kuangusha mabomu katika msitu wa Boni ambapo wanamgambo wa kundi hilo la Kiislamu wanadaiwa kujificha.
Wakazi waliokuwa wakiishi msituni na karibu na msitu huo walitakiwa kuhama.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *