Home / Habari za Kimataifa / Catalonia ‘yapata haki ya kuwa huru’

Catalonia ‘yapata haki ya kuwa huru’

Catalonia ‘yapata haki ya kuwa huru’
Kiongozi wa eneo la Catalonia Carles Puigdemont anasema kuwa eneo la Uhispania limepata haki ya kuwa huru kufuatia kura ya maoni yenye utata ambayo imekubwa na ghasia.
Alisema kuwa sasa mlango umefunguliwa kwa eneo hilo kutangazwa kuwa huru.
Maafisa wa Catalonia baadaye walisema kuwa asilimia 90 ya wale walioapiga kura waliunga mkono uhuru kwenye kura ya maoni ya siku ya Jumapili.
Zaidi ya 300 wajeruhiwa wakati wa kura ya uhuru Catalonia
Mahakama ya katiba nchini Uhispania imeitangaza kuta hiyo ya maoni kuwa iliyo kinyume na sheria na mamia ya watu walijeruhiwa wakati polisi walitumia nguvu kujaribu kuzuia zoezi hilo.

Kiongozi wa neo la Catalonia Carles Puigdemont anasema kuwa eneo la Uhispania limepata haki ya kuwa huru
Polisi walichukua makaratasi ya kupigia kura na masanduku kutoka kwa vituo vya kupigia kura.
“Siku hii ya leo ya matumaini na mateso, watu wa Catalonia wameshinda haki yao ya kuwa na taifa huru kama jamhuri,” Bw Puigdemont alisema alipotoa hotuba kupitia televisheni akiandamana na maafisa wengine wa vyeo vya juu wa Catalonia.
Wapiga kura wataka Catalonia kujitenga
“Serikali yangu kwa muda wa siku chache zinazokuja itatuma matokeo ya kur ya leo kwemda kwa bunge la Catalonia, ili ifanye kuambatana na sheria ya kura ya maoni.”

Mwanamke huyu alipata jereha la kichwa huko Barcelona

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *