Ujasiriamali

Teknolojia ya matone kuinua wakulima

WAKULIMA 5,000 wa mboga wilaya ya Same, wanatarajia kubadili mfumo wa maisha yao kwa kuwa wajasiriamali wakubwa na kuendesha kilimo bora cha umwagiliaji wa matone kwa teknolojia rahisi kwa watu wa kada zote.

Kilimo hicho kinatumia dumu lenye maji na mipira midogo ya maji na kusambaza katika tuta la mboga lenye miche zaidi ya 80 ya mboga kama chinese, mnavu, mchicha.

Akizungumzia mradi huo, Mkuu wa wilaya ya Same, Rosemary Senyamule ambaye ameahidi kuwa na matuta 10 ya mbogamboga nyumbani kwake na moja nje ya eneo la ofisi yake, alisema gharama za miundombinu ni 27,500 kwa tuta moja.

Alisema tayari kata za Bombo na Mtii zimefundishwa teknolojia hiyo kutoka shirika la Kikristo Tanzania (CCT) na baadaye kusambazwa katika kata zote 34 za wilaya hiyo. “Wilaya imekusudia kuwawezesha wajasiriamali wa mboga kuitumia barabara kuu ya Arusha/Dar es Salaam kuuza mbogamboga na hata mazao mengine kama tangawizi ambayo inalimwa kwa wingi katika wilaya yetu,” alisema

Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close