Home / Habari Za Kitaifa / KAMA MZAZI: ADHABU MBADALA WA FIMBO NAYO…

KAMA MZAZI: ADHABU MBADALA WA FIMBO NAYO…

NIKIWA katika mapumziko ya jioni katika moja ya maeneo ya kujidai jijini Dar es Salaam nilikutana na jamaa yangu mmoja ambaye tulikua katika kijiji kimoja na kusoma pamoja shule ya msingi na kisha kwenda sekondari pamoja.

Tulikumbushana mengi sana ya utoto wetu pamoja na maisha ya shule nyakati hizo tukilinganisha na tunayoshuhudia hivi sasa kwa watoto wetu wa kizazi cha dotikomu. Mazungumzo yetu yalisindikizwa na vinywaji pamoja na vitafunwa lukuki tulivyoweza kupata katika eneo hilo la burudani.

Lakini kilichonikumbusha zaidi na kuona ni muhimu wasomaji wangu wa safu hii kuwamegea ni pale aliponisimulia adhabu aliyowahi kupewa na baba yake mzazi ambayo alisema hataisahau. Anasema, aliadhibiwa baada ya kukaidi kwa muda wa siku nzima kila alichokuwa anatumwa na mama yake mzazi, kuanzia kwenda dukani, kuchota maji hadi kufua nguo zake mwenyewe.

Nilimsikiliza kwa makini kwa kutaka kujua aina ya adhabu aliyopewa kwani nilihisi kwamba haitakuwa adhabu ile ambayo watu huwa tunaifahmu kwa haraka haraka kwa watoto wakaidi ya kuchapwa bakora hasa mama anaposhitaki kwa baba baada ya mtoto kuwa mkaidi.

“Sikufahamu mara moja sababu hasa ya siku hiyo kuwa jeuri kiasi hicho lakini nilikataa kufanya karibu kila nilichotumwa,” anasema. Anasema, baba yake aliporejea kutoka shambani mama yake hakupoteza muda akamweleza mkanda wote uliotokea siku hiyo na akawa tayari kusubiri kuitwa wakati wowote ule ili kuadhibiwa lakini hilo halikutokea na badala yake alitumwa kumfukuza jogoo na kisha kumpeleka kwa baba yake amchinje.

Alipokamilisha kazi hiyo alikwenda kucheza kwa watoto wenzake na kwamba bahati mbaya wakati huo ulikuwa wakati wa shida ya chakula hivyo ilikuwa ni vigumu kwa familia kupata chakula walichokipenda hasa wali. Nyakati hizo wengi walikuwa wanakula ndizi za kuchemsha au ugali nyakati za jioni kinyume na mila na desturi za watu wanaoishi katika kijiji walichoishi.

‘’Nilivyorudi mchezoni nilikuta mama kishapika kuku na alikuwa katika pilikapilika ya kupika wali…tangu wakati huo sikucheza mbali kiasi cha kwamba wakati mwingine nilihisi mama ananiita kumbe ni fikra zangu tu,” anasema. Anasema, nyumbani kwao walikuwa na desturi za watoto wote kukusanyika pamoja na kula chakula kutoka kwenye sahani kubwa.

Wakati ulipowadia wa kuandaliwa chakula aliitwa na kukifikisha mahali alipoketi baba yake na kisha wote walikusanyika na baada ya kusali wakaanza kula. ‘’Nilimega tonge la kwanza na kulisokomeza kinywani kwa haraka, ukizingatia kwamba siku hiyo ilikuwa chakula kizuri, wali kwa kuku lakini wakati najiandaa kuchukua tonge la pili, baba alinisimamisha na kuniambia sistahili kuendelea kula siku hiyo kutokana na jeuri niliyomfanyia mama mchana.

SOURCE HABARI LEO

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *