Home / Habari Za Kitaifa / Wazee ni hazina yetu, tuwatunze na kuwaenzi

Wazee ni hazina yetu, tuwatunze na kuwaenzi

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega amekabidhi kadi ya bima ya Afya kwa mmoja wa wazee aliowakatia bima ya afya ikiwa ni moja ya ahadi zake kwa wananchi wa jimbo lake katika Mkutano uliofanyika Mkuranga.

Ulega aliwaeleza wananchi katika mkutano huo kuwa zaidi ya shilingi bilioni 1.2 zimetengwa na Wakala wa barabara nchini TANROAD kwa ajili ya ujenzi wa barabara kutoka Ulanga hadi Kurungu wilayani Mkuranga katika mkoa Pwani.

“Ndugu zangu wanamkuranga mwanenu napambana kwelikweli kwa maana najua niliahidi na nyie mlinituma na mmeendelea kunituma nami staki kuwaangusha hivyo kuanzia January hadi Februari mwaka huu 2018 ujenzi wa barabara hii ambayo nimetaja ujenzi wake utaanza mara moja,”alisema Ulega huku wananchi hao wakifurahia na kushangilia.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *