Habari Za KitaifaUchumi na Biashara

Zabibu Dhahabu ya Dodoma

KITUO cha Utafiti cha Makutupora (TARI) jijini Dodoma kimepewa Sh milioni 400 kwa ajili ya kupanua huduma za utafiti wa zao la zabibu mkoani humo na katika maeneo mengine nchini.

Kituo hicho kinachofanya kazi chini ya Wizara ya Kilimo, ni maalumu kwa ajili ya utafiti wa zao zabibu, aina zake, maeneo na ardhi inayofaa kwa ajili ya uzalishaji zao ili hilo ili kuleta tija na faida kwa wazalishaji.

Akizungumza katika kikao cha kuzindua Kamati ya Tamasha la Mvinyo, Mtafiti wa kituo hicho, Amachius James amesema fedha hizo zilizotengwa zinalenga kuongeza, kupanua na kukuza utafiti katika zao hilo ili kuongeza uzalishaji kwa wakulima.

“Kutokana na kupatikana kwa fedha hizo, utafiti wetu utawapa wakulima mbalimbali wa zao hilo, kuleta sampuli za zabibu wanazozalisha ili kuona ni namna gani zinaweza kuboreshwa ili kuzaa mazao mengi zaidi,”amesema.

James alisema pia fedha hizo zitasaidia kuongeza fursa ya kufanya utafiti aina bora ya zabibu au mvinyo gani unaoweza kutoa juisi nyingi na bora, ili kuhakikisha wakulima aina ya zao na maeneo wanayoweza kulima ili kupata zabibu na juisi nyingi zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amesema zao la zabibu ndiyo dhahabu ya kuutambulisha mkoa wa Dodoma, hivyo tamasha hilo linaloandaliwa litakuwa fursa adhimu ya kuitangaza rasilimali hiyo pamoja na vivutio vingine.

Uzalishaji wa zabibu ulianza miaka 150 iliyopita, ulififia miaka ya 1990, lakini sasa mkakati uliopo ni kuhakikisha wakulima wanahamasishwa kuzalisha na wawekezaji wakiwemo sekta binafsi wanashiriki katika kujenga viwanda ili wazalishaji wawe na soko la uhakika wa zao lao.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge alisema Tamasha la Mvinyo limekuja wakati muafaka ambapo mkoa umeweka mkakati wa kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo mkoani zikiwamo zabibu na mvinyo.

Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Mvinyo, Iddi Senge ambaye ni Mwakilishi wa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) amesema, sekta binafsi itakuwa bega kwa bega kushirikiana na serikali na hasa watafiti kwa karibu katika kuboresha mnyororo wa thamani wa zao.

Tags
Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close