Makala

Jakarta, mji unaozama kwa kasi ya juu zaidi duniani

Mji mkuu wa Indonesia Jakarta ni nyumbani kwa watu milioni 10 lakini mji huo pia unazama kwa kasi zaidi duniani. Ikiwa hatua hazitachukuliwa sehemu za mji huo mkubwa huenda zikazama kabisa ifikapo mwaka 2050 kwa mujibu wa watafiti.

Mji huo uko eneo lenye kinamasi kando mwa bahari, huku mito 13 ikipita kwenye mji huo na hivyo sio jambo la kushangaza kuwa mafuriko ni jambo la kawaida mjini Jakarta kwa mujibu wa wataalamu, hali inayozidi kuwa mbaya na mji huo ukizidi kutoweka.

Kaskazini mwa Jakarta unazama kwa sintimita 25 kila mwaka

“Uwezekano wa Jakarta kuzama sio jambo la kufanyiwa mzaha,” anasema Heri Andreas, ambaye amechuguza kutokewa kwa ardhi kwenda mjini Jakarta kwa miaka 20.

“Tukiangangalia uchunguzi wetu ifikapo mwaka 2050 karibu asilimia 95 ya eneo la Kaskazini mwa Jakarta litakuwa limezama.

Heri Andreas anaonyesha ukuta uliojengwa kuzuia maji ya bahari kufurika nyumba

Tayari inafanyika – eneo la Kaskazini mwa Jakarta limezama mita 2.5 katika kipindi cha 10 na linazidi kuzama kwa karibu sintimita 25 kwa mwaka sehemu zingine.

Jakarta huzama kwa kasi ya sentimita 1-15 kwa mwaka na karibu nusu ya mji uko chini ya bahari.

Athari tayari zimeonekana Kaskazini mwa Jakarta.

Kwenye wilaya ya Muara Baru, jengo lote la ofisi limebaki mahame. Awali ilikuwa ni kampuni ya uvuvi lakini ghorofa ya kwanza ndiyo tu inaweza kutumiwa.

Sehemu ya kwanza ya jengo sasa iko ardhini

Sehemu ya kwanza sasa imebaki kufurika maji. Ardhi inayozunguka iko juu kwa hivyo maji hayawezi kutoka.

Maji yaliyokwama chumba cha chini

Mwaka baada ya mwingine ardhi imekuwa ikizama.

Eneo la Kaskazini mwa Jakarta lina historia ya bandari na hata sasa ndiyo ilipo bandari yenye shughuli nyingi zaidi chini Indonesia, Tanjung Priok.

Leo hii watu 1.8 wanaishi eneo hilo.

Fortuna Sophia anaishi kwenye nyumba ya kifahari, kuzama kwa nyumba yake hakuwezi kuonekana mara moja lakini anasema nyufa huonekana kwenye kuta na nguzo kila baada ya miezi sita.

Fortuna

Ameishi hapa kwa miaka minne lakini eneo hjlo mara kadhaa limefurika: ” Maji ya bahari huinga na kufurika kabisa kidimbwi cha kuogelea. Inatubidi tuhamishe kila kitu kwenda ghorofa ya kwanza.” anasema

Athari kwa nyumba ndogo karibu na bahari zinaonekana. Wakaazi ambao wakati mmoja walikuwa wanaiona bahari kwa sasa wanaona ukuta uliojengwa kuzuia maji ya bahari.

“Kila mwaka maji ya bahari hupanda sentimita 5,” mvuvi Mahardi anasema.

Ramani ya Indonesia na Jakarta

Maeneo mengine ya Jakarta nayo yanazama kwa mwendo wa chini. Magharibi mwa Jakarta, ardhi inazama kwa karibu sentimita 15 kwa mwaka, kwa sentimita 10 mashariki, sentimita 2 kati kati mwa Jakarta na sentimita 1 kusini mwa Jakarta.

Miji iliyo pwani kote duniani imeathiriwa kutokana na kupanda kwa viwango vya bahari kufuatia na mabadiliko ya hali ya hewa, Kuongezeka kwa viwango vya bahari husababisha kuongezeka kwa joto na kuyeyuka kwa theluji. Kasi ya kuzama kwa mji wa Jakarta imewatia wasiwasi wanasayansi.

Kuzama kwa mji wa Jakarta kumetokana na kutumika kwa maji wa chini ya ardhi kupitia uchimbaji visima kwa kunywa, kuoga na matumizi mengine ya kila siku miongoni mwa wakaazi wa mji.

Maji ya mifereji hayapatikani sehemu zingine kwa hivyo watu hawana lingine ila kutafuta maji mbali zaidi chini ya ardhi.

Wengi wa wakaazi wa Jakarta hutegemea maji ya visima

Hendri, mmiliki mmoja wa nyumba huko Jakarta ana jumba la makaazi linalofahamika kama kos-kosan na amekuwa akitumia maji ya kisima kwa miaka 10 kwa wapangaji wake. Ni mmoja kati ya wamiliki wengi ya nyumba wanaofanya hivyo.

“Ni vizuri tutumie maji yetu kuliko kutegemea mamlaka . kos kosan uhitaji maji mengi.”

Manispaa moja hivi karibuni ilikiri kuwa visima haramu vimekuwa tatizo.

Mwezi Mei mamlaka za mji wa Jakarta zilikagua majengo 80 kati kati mwa Jakarta, mtaa wa Jalan Thamrin kwenye majengo marefu, maduka na mahoteli. Iligundua kuwa majengo 56 yana visima vyao na 33 yalifanya hivyo bila vibali.

Iligundulika kuwa majengo 56 yana visima vyao na 33 yalifanya hivyo bila vibali.

Mamlaka pia zinamatumani kuwa Great Garuda, ukuta wa umbali wa kilomita 32 unaojengwa Jakarta utasaidia kuukoa mji huo kuzama kwa gharama ya dola bilioni 40.

Ukuta huu na kuzuia mafuriko mjini

Jan Jaap Brinkman mtaalamu anayefanya kazi na taasisi za maji huko uholanzi anasema suluhu ni kuzuia matumizi ya maji ya visima na kutegemea vyanzo vingine vya maji kama mvua na mito.

Ujenzi wa ukuta wa bahari unaendelea

Anasema Jakarta ni lazima ifanye hivyo ifikapo mwaka 2050 kuzuia mji kuzama zaidi.

Vyanzoa vingine vya maji kama mito imechafuka sana

Sio ujumbe ambao unatiliwa maanani na Gavana wa mji wa Jakarta Anies Baswedan anasema njia nyingi inaweza kusaidia.

Anasema watu wanaweza kutumia maji ya visima kisheria kama wanaweza kurejesha maji hayo tena ardhini kwenye mfumo unaojulikana kama biopoli.

Hapa ni wakati mtu anachimba shimo la upana wa sentimita 10 na lenye kina cha sentimita 100 kuruhusu maji kurudi tena ardhini.

Ukuta unaozuia maji karibu na bahari

Kuna teknolojia ya kurejesha maji ya visima kwenye vyanzo vyake lakini ni ghali mno. Tokyo ulitumia mfumo huu wakati ardhi yake ilishuka sana miaka 50 iliyopita. Serikali pia ikadhibiti matumizi ya matumizi ya maji ya visima na biashara zikaaza kutumia maji ya mifereji. Kushuka kwa ardhi kukasitishwa.

Rais Joko Widodo anasema itachukua miaka mingi kusafisha mito ya Jakarta

Taarifa zaidi na Tom de Souza. michoro na Arvin Surpriyadi, Davies Surya, na Leben Asa.

Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close