Home / Afya / Je wajua kwamba nguo za kubana huathiri ‘mbegu za kiume’?

Je wajua kwamba nguo za kubana huathiri ‘mbegu za kiume’?

Kaptula ya ndani kama iliyovaliwa na Gary Lineker kwenye mechi ambayo Leicester City ilichukua ubingwa wa ligi kuu uhusishwa na idadi ya mbegu za kiume

Kuvaa nguo za ndani zilizo pana kunaweza kuwa njia rahisi kwa wanaume kuimarisha mbegu za kiume na homoni zinazozidhibiti, utafiti uliofanyika nchini Marekani umeeleza.

Utafiti uliowahusisha wanaume 656, uliofanywa na Chuo cha masuala ya afya cha Havard TH Chan nchini Marekani, wanaovaa boxer zilizo kubwa walikuwa na ongezeko kwa 25% ya ubora wa mbegu za kiume kuliko wanaume wanaovaa nguo za ndani zinazobana.

Kutokuwepo kwa hali ya joto kwenye maungo ya kiume kunaweza kuwa sababu.

Wataalamu wanasema mtindo huu rahisi wa maisha unaweza kuboresha uzazi wa wanaume.

‘Ubongo husaidia uzalishaji wa mbegu za kiume’

Uzalishaji wa mbegu za kiume haupendelei joto la zaidi ya nyuzi 34C, ndio maana korodani huning’nia kando ya mwili

Baadhi ya mitindo ya nguo za ndani, za kubana kama nguo za waendesha farasi, hubana maumbile hayo na kusababisha kutokea hali ya joto, huku mavazi ya ndani ambayo hayabani hufanya maumbile hayo kupata hewa ya kutosha.

Watafiti wamebaini kuwa wanaume wanaokwenda hospitali kwa ajili ya masuala ya uzazi wakiwa wamevaa nguo za ndani zisizobana wanakuwa ongezeko la ubora wa mbegu za kwa 17% .

Hata hivyo,maumbo ya mbegu hizo haziathiriwi wala ubora wa vinasaba vyake.

Pia watafiti walizingatia vitu kadha wa kadha ambavyo vinaweza kuathiri mbegu za kiume ikiwemo, Umri, uzito wa mwili na tabia kama kuvuta sigara, mazoea ya kutumia maji ya moto kwenye mabeseni ya kuogea vyote vinakisiwa kuwa joto lake linaweza kuwa chanzo cha tatizo.

Utafiti umebaini kuwa homoni zilizo kwenye ubongo zenye kazi ya kuziambia korodani kutengeneza mbegu za kiume, huitwa follicle stimulating hormone zilikuwa chini kwa 14% kwa wale wanaovaa nguo za ndani zisizobana.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

WANAWAKE WATAKIWA KUNYONYESHA WATOTO MAZIWA YAO PEKEE

WANAWAKE wametakiwa kunyonyesha watoto maziwa ya mama pekee bila kuwapa maji, kinywaji au chakula kingine …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *