Uchumi na Biashara

SOKO LA VIUNGO LA UHAKIKA NJE YA NCHI

WIZARA ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi imewataka wakulima wa mazao ya viungo kuongeza juhudi ili kuzalisha zao la vanila ambalo soko lake lipo kubwa la uhakika nje ya nchi.

Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Rashid Ali Juma amesema hayo wakati akizungumza kuhusu mikakati ya wizara kuzalisha mazao ya viungo ambayo mahitaji yake ya soko ni makubwa nje ya nchi.

Amesema tayari Wizara ya Kilimo kwa kutumia mabwana shamba na wataalamu wake imeanzisha mashamba ya majaribio kwa ajili ya kuotesha zao la vanila eneo la Kizimbani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Amesema, utafiti umefanywa na kuonesha kwamba Zanzibar mazao hayo yanastawi kwa wingi na kuweza kuleta tija kwa wakulima.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, soko la zao la vanila lipo katika nchi ya China pamoja na Bara Hindi na Arabuni kwa ajili ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo za vyakula.

“Tumehakikishiwa soko la bidhaa mazao ya vanila katika nchi ya China na Bara Hindi kwa hivyo wakulima kazi kwenu katika kuzalisha mazao hayo kwa mafanikio makubwa,” amesema.

Kwa mfano amesema tani moja ya vanila inauzwa kati ya Dola za Marekani 700 hadi 900, kiwango ambacho kinaweza kumkomboa mkulima wa mazao ya viungo.

Aidha ameyataja mazao mengine ya viungo ambayo soko lake lipo la uhakika kuwa ni pilipili manga, bizari nyembamba, hiliki pamoja na pilipili hoho.

Visiwa vya Zanzibar katika miaka ya 1960 vilikuwa maarufu kwa uzalishaji na usafirishaji wa mazao ya viungo ikiwemo karafuu, mbata ambayo hutumika kwa ajili ya uzalishaji wa mafuta ya nazi.

Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close