Habari za KimataifaImani

Saudi Arabia Yajiandaa Kwa Hijja

Saudi Arabia inajiandaa kuwapokea mahujaji wanaoshiriki kwenye Hijja. Mwaka huu Hijja inaanza kesho Jumapili. Zaidi ya waumini milioni 1.6 wa Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali duniani wamekwisha wasili nchini humo. Hijja ni moja kati ya nguzo tano za Kiislamu na ni muhimu kwa kila Muislamu anayejiweza kwenda kuhiji angalau mara moja katika maisha yake. Katika wiki za hivi karibuni Waislamu wamekuwa wakiwasili katika mji mtakatifu wa Makkah. Hijja inatoa fursa kwa mahujaji kujihisi wapo karibu na Mungu katika wakati ambapo ulimwengu ukikabiliwa na changamoto nyingi ambazo ni pamoja na kitisho cha waislamu wenye itikadi kali katika eneo la mashariki ya Kati.

Tags
Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close