Home / Afya / DAKTARI- KIPIMO CHA MIONZI HAKIPUNGUZI UMRI

DAKTARI- KIPIMO CHA MIONZI HAKIPUNGUZI UMRI

Daktari Bingwa wa Radiolojia kutoka Taasisi ya Mifupa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI), Mechris Mango amesema, kuna baadhi ya watu wanahofu kupima kipimo hicho cha picha kwa madai kuwa kinasababisha mtu kupunguza umri wa kuishi jambo ambalo si kweli.

Amesema kuna kiwango kikifikia ndio inaweza kusababisha mionzi lakini vipimo vya sasa vimewekwa katika mfumo ambao hauwezi kufikia katika kiwango cha madhara.

“Haiwezekani mtaalamu anayepima kipimo hicho kufikia kiwango chenye madhara kwa mpimwaji, mashine za sasa zimetengenezwa kwa namna ambayo hazitaruhusu na kabla ya kufikia huko zinatoa mlio wa tahadhari.

“Ni kama gari, unapoendesha ikiisha mafuta itakuwashia taa kukupa tahadhari halitazimika tu, na mashine zetu ni hivyo ukipitiliza utapata mlio kukuashiria unakoelekea huko sio salama na haitakuruhusu kuendelea ukibonyeza haiendi,” amesema Dk Mango.

Amesema hata hivyo kuna mionzi hatari kila mahali, kwenye jua, rangi za nyumba, kwenye dunia lakini mionzi ya kwenye kipimo imedhibitiwa katika mashine zake.

Amesema, kuna bodi zinazosimamia mionzi hiyo iliyoko kwenye vipimo vya X-ray isiwe na madhara kwa binadamu kuhakikisha kwamba mionzi inayotolewa ni salama kwa na pia wanaotumia mashine hizo wanafundishwa.

Alisema matangazo yaliyopo kwenye nyumba vya X-ray kuwataka watu wasikae eneo hilo ni kwa tahadhari tu kwa kuwa eneo hilo wakati wote mashine zinafanya kazi.

“Tunachoambiwa ni mionzi inaweza kuleta madhara sasa hayo madhara ndiyo yanayoweza kufupisha maisha, ukiwa na kansa lazima maisha yatapungua”amesema.

Dk Mango amesema kipimo hicho hakipunguzi umri wa mtu kuishi bali ni kwa sababu vipimo hivyo vina mionzi ambayo inaweza kusababisha mgonjwa kama saratani

“Sio kwamba mionzi hiyo inaua au inapunguza umri wa kuishi bali mionzi inaweza kukusababishia maradhi kama saratani kwa hiyo ukiwa na ugonjwa ambao hautibiki si unapunguza umri wa kuishi,” amesema.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Je wajua kwamba nguo za kubana huathiri ‘mbegu za kiume’?

Na Lucy R GreenScience fellow Kaptula ya ndani kama iliyovaliwa na Gary Lineker kwenye mechi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *