Michezo

Kocha Wa Simba Akiri Udhaifu

Simba Sports Club Coach
Licha ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Simba kuanza michuano hiyo vizuri kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons juzi, kocha wake Patrick Aussems amesema safu yake ya ushambuliaji ilikosa ufanisi. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, alisema walitengeneza nafasi nyingi za kufunga hasa kipindi cha pili lakini walikosa ufanisi katika kuzitumia.

“Mchezo ulikuwa ni mgumu tunashukuru tulianza vizuri kwa bao la mapema, tulitengeneza nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia kwa kukosa ufanisi lakini tutaendelea kuboresha kwa ajili ya michezo ijayo,” alisema. Aussems alisema pia kuwa walijua wazi mapema mpinzani wao ni watu wa aina gani, kwani nao walicheza vizuri licha ya kwamba walishindwa kupenyeza kwao kiurahisi kutokana na ubora wa safu yake ya ulinzi. Alisema jambo muhimu ni kwamba wameanza vizuri bila kufungwa na sasa wanaangalia zaidi mbele katika mchezo ujao dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Jumamosi kwenye uwanja huo.

Kwa upande wa kocha wa Prisons, Mohamed Abdallah aliwapongeza wapinzani wake Simba kwa kupata pointi tatu na kusifia kuwa mchezo ulikuwa mzuri kwa kuwa timu zote zilijiandaa na mwisho wa siku mmoja akaibuka mshindi. Alisema kikosi chake kina baadhi ya wachezaji wageni waliosajiliwa msimu huu hawajazoea, lakini kadiri siku zitakavyosogea anaamini watabadilika.

“Tuliondokewa na wachezaji wenye uzoefu kama Eliuter Mpepo na Mohamed Rashid na sisi tuliziba nafasi kwa kuingiza wengine, tunaamini watazoea taratibu kama hao na kufanya vizuri,” alisema. Katika mchezo huo, ilipata bao hilo pekee katika dakika ya kwanza lililofungwa na Meddie Kagere, lakini walibanwa katika kipindi cha pili na kushambuliwa mara kwa mara.

Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close