Home / Michezo / Samatta Apiga Hatrick Genk

Samatta Apiga Hatrick Genk

Mkali wa mabao wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameendelea kuwatesa wazungu kwa kuzifumania vyavu, baada ya juzi usiku kupiga mabao matatu wakati Genk iliposhinda 5-2 dhidi ya Brondly. Samatta alifunga mabao hayo dakika ya 37, 55 na 70, ukiwa ni mchezo wa kufuzu mashindano ya Ligi ya Ulaya na kufanya kuwa na mabao matano katika hatua hiyo akicheza michezo mitatu.

Mshambuliaji huyo amekuwa na msimu mzuri tangu kuanza kwa Ligi Kuu ya Ubelgiji kwani pamoja na kufunga mabao hayo, Samatta alifunga mabao mawili katika mchezo wa Ligi dhidi ya Sporting Charleroi. Baada ya kupiga mabao hayo, Samatta anafikisha jumla ya mabao saba ndani ya michezo mitano ya mashindano ya Ligi na ile ya kufuzu Ulaya.

Furaha ya Samatta aliionesha baada ya kumalizika kwa mchezo huo, ambapo alisema baada ya hat trick hiyo nyingine nyingi zitafuata. “Nina furaha kufunga hat trick yangu ya kwanza nikiwa na Genk, nina imani nyingine nyingi zitafuata haina kufeli,”alisema Samatta. Baada ya ushindi huo, Genk itasafiri mpaka Denmark kwenye dimba la Brondly Stadio kwa ajili ya mchezo wa marudianio utakaopigwa Agosti 30, baada ya mchezo wa Jumapili hii, ambapo Genk itacheza mchezo wa Ligi dhidi ya Waasland-Beveren.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *