Michezo

Tetesi za Soka Ulaya

Mourinho

Wachezaji, wakufunzi na wafanyakazi wengine wa Manchester United wanaamini Jose Mourinho atafutwa kazi iwapo atashindwa mechi nyingine moja. (Daily Mail)

Maafisa wakuu wa klabu hiyo hata hivyo bado wana imani kwamba Mourinho, 55, anaweza kubadilisha mambo katika klabu hiyo hata baada ya United kushindwa mechi mbili kati ya tatu za kwanza Ligi ya Premia kwa mara ya kwanza tangu 1992-93.

Real Madrid wanamtaka mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling, 23, ambapo klabu hiyo ya La Liga inatarajiwa kumfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa England uwanjani Wembley akicheza mechi ya Ligi ya Mataifa ya Uefa mnamo 8 Septemba. (Sky Sports)

Winga wa Liverpool Sheyi Ojo, 21, anakaribia kujiunga na klabu ya Stade de Reims ya Ufaransa kwa mkopo kwa kipindi kilichosalia msimu huu. Hii ni baada ya raia huyo wa England kueleza nia ya kutaka kuhamia ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1. (Mirror)

Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester City Yaya Toure, 35, anakaribia kujiunga na klabu moja ya London. Hii ni baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Ivory Coast kupitia vipimo vya kiafya, wakala wake amesema. (Twitter)

Real Sociedad wanataka kumchukua mshambuliaji wa Everton raia wa Uhispania Sandro Ramirez. Mchezaji huyo wa miaka 23 alihamia Goodison Park majira ya joto yaliyopita lakini akatumwa Sevilla kwa mkopo. (Marca)

Tottenham wawafunga Man Utd Old Trafford
Jedwali la Msimamo wa ligi ya EPL 2018/19
Fenerbahce wamekanusha taarifa kwamba wanajaribu kumnunua kiungo wa kati wa Tottenham raia wa Ufaransa Moussa Sissoko, 29. (Sky Sports)

Sterling akisherehekea kushinda ligi akiwa na mpenzi wake Paige na mwana wao wa kiume Thiago
Winga Lucas Moura, 26, amesifiwa sana kama mmoja wa wachezaji muhimu zaidi Tottenham kwa sasa baada ya Mbrazil huyo kukaa Paris St-Germain kwa mkopo. Moura alifunga mabao mawili dhidi ya Manchester United Jumatatu wiki hii. (Sports Illustrated)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alitaka kumnunua mchezaji huyo wa Spurs kwa mujibu wa wakala wa Moura. (Manchester Evening News)

Beki wa zamani wa Manchester United Paul Parker, 54, anasema meneja wa sasa wa klabu hiyo Jose Mourinho anafaa kuihama klabu hiyo baada yao kushindwa 3-0 na Tottenham nyumbani Jumatatu. (Talksport)

Mkabaji wa Barcelona Gerard Pique, 31, amesema hawezi kamwe kurejea Manchester United. Mhispania huyo aliondoka Old Trafford na kuhamia Nou Camp mwaka 2008. (Star)

Beki wa Chelsea Cesar Azpilicueta, 29, anafahamu ni wapi Blues wanahitaji kujiimarisha licha ya klabu hiyo kushinda mechi zao tatu za kwanza msimu huu. (Football.London)

Kipa wa England Jordan Pickford, 24, anasema wachezaji wa Everton wameanza kukumbatia na kuuamini mtindo wa uchezaji wa meneja wao Marco Silva. (101 Great Goals)

Meneja wa Roma Eusebio Di Francesco anahitaji kufanyiwa upasuaji kwenye mkono wake wa kushoto baada yake akiumia akisherehekea bao la kusawazisha dhidi ya Atalanta siku ya Jumatatu. (Daily Mail)

Meneja wa Newcastle United Rafael Benitez anasema hajazozana kwa vyovyote vile na beki wa klabu hiyo raia wa England Jamaal Lascelles, 24, ambaye pia ni nahodha wa klabu hiyo inayochezea St James’ Park. (Goal)

Beki wa Uhispania na Barcelona Gerard Pique, 31, anasema itakuwa vyema sana iwapo kiungo wa kati wa Manchester United aliyeshinda Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa Paul Pogba, 25, atahamia Nou Camp siku zijazo. (AS)

Beki wa England anayechezea Chelsea Gary Cahill, 32, yuko tayari kusalia na kupigania nafasi yake baada ya kuonekana kuwekwa pembeni katika kikosi cha Maurizio Sarri. (Telegraph)

Chimbuko la mchezaji Paul Pogba
Unaweza kumtambua Pogba kati ya wawili hawa?
Pogba: Mourinho aliniambia nijisikie huru uwanjani
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Ufaransa Thierry Henry, 41, anatarajiwa kuikataa nafasi ya kuwa meneja wa Bordeaux kwa sababu ya wasiwasi kuhusu ukosefu wa fedha katika klabu hiyo ya Ligue 1. (Sun)

Beki wa West Ham Reece Oxford, 19, anatafutwa kwa mkopo na klabu ya Eibar inayocheza ligi kuu Uhispania, klabu ambayo iko tayari kulipa ada ya £1.8m ya uhamisho wa mkopo. (Marca)

Kiungo wa kati wa zamani wa Chelsea na Brazil Ramires, 31, anakaribia kurejea klabu yake ya zamani ya Benfica kwa mkopo kutoka klabu ya China ya Jiangsu Suning. (O Jogo)

Aston Villa wanajaribu kumshawishi mshambuliaji wa England Jack Grealish, 22, atie saini mkataba wa kudumu katika klabu hiyo inayocheza ligi ya Championship baada yao kukataa kumuuza Agosti.

Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close