AfyaHabari za Kimataifa

Daktari; Matumizi ya kucha na kope bandia yana madhara

Wakati mjadala wa matumizi ya kucha na kope bandia ukirindima nchini Tanzania, daktari kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) ameimbia BBC kuwa matumizi ya urembo huo yana athari kiafya.

Mjadala kuhusu urembo umeibuka Jumatatu mara baada ya Spika wa Bunge la Tanzania kupiga marufuku wanawake (wabunge na wageni) kuingia bungeni wakiwa wamebandika kucha na kope bandia akitaja sababu za kiafya.

Hatua hiyo ya Spika Job Ndugai imeibua mjadala mkubwa huku watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wakimkosoa.

Mwandishi wa BBC Munira Hussein amezungumza na daktari Fredrick Mashini ambaye pia ni mhadhiri wa Muhas na kutaka kujua athari za urembo huo bandia.

Dk. Mashini ameimbia BBC kuwa ni kweli urembo huo una madhara yanayotofautiana kulingana na ubora wa bidhaa (kope na kucha bandia) na kiwango cha utumiaji.

Kwamujibu wa daktari, matumizi ya kope bandia ndio hatari zaidi sababu yanahusisha kiungo muhimu cha jicho.

Moja ya tatizo ambalo limewakuta wengi linatokana na gundi inayotumika kupachika kope hizo bandia,”gundi ile inakuwa imeshika sana kwa hiyo wakati wa kutoa inasababisha zile kope halisi kunyofoka, kitu ambacho si kizuri kwa afya.”

“Bidhaa zipo za aina nyingi, kwa hiyo kuna ambazo zina ubora duni na nyingine ni nzuri na hazina madhara. Ushauri ni kuwa, mtu hatakiwi kutumia kwa muda mrefu, akaenazo siku moja kisha azitoe.”

Tatizo jingine kubwa linalotokana na matumizi ya kope bandia ni kukusanya uchafu na vijidudu ambavyo vinaweza kuathiri jicho.

“Kwasababu zinakuwa ni ndefu na nyingi zaidi, huwa zinakamata vijidudu ambavyo vinaweza kusababisha magonjwa.”

Kwenye upande wa kucha bandia Dk. Mashini amesema athari zake si za hatari ka ma ilivyo kwa kope. “Kwa kucha pia inategemea ubora wake na vitu vilivyotumika katika kubandika ambapo mtu akikosea tu huathiri kucha ya asili.”

BBC imetembelea mitaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam na kuzungumza na baadhi wa watumiaji wa kucha na kope bandia pamoja na wale wenye maduka ya bidhaa hizo.

Mmoja wa kijana anayebandika wanawake kope bandia Hamisi Omari ameimabia BBC kuwa anapata wateja wengi kila siku na hakuna hata mmoja aliyewahi kurudi na kulalamika kuumwa macho.

“Nimetumia urembo huu kwa muda mrefu sasa na sijawahi kuumwa. Nimeshasikia kuwa kope bandia zina madhara lakini siwezi kuacha kwasababu sijawahi athirika,” mmoja wa watumiaji wa urembo huo ameiambia BBC.

“Mimi naweka kucha bandia tu, siwezi kuweka kope. Naogopa ile gundi. Macho ni tofauti na kucha… siwezi kujaribu,” amesema mtumiaji mwengine wa urembo huo.

Show More

komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close