Home / Habari za Kimataifa / Kimbunga Florence kimesababisha watu kukimbia makazi yao Marekani

Kimbunga Florence kimesababisha watu kukimbia makazi yao Marekani


Kimbunga Florence chawa tishio Marekani

Majimbo kadhaa nchini Marekani yametangaza hali ya hatari kufuatia kufuatia kimbunga Florence kudaiwa kuelekea pwani ya mashariki mwa taifa la hilo.Takribani watu milioni 1.7 wana yahama maeneo yao kwa hiari na wengine kwa amri maalumu ili kuepuka madhara ya kimbunga hicho.

Kimbunga hicho kinasafiri kwa kilomita 195 kwa saa,huku mawimbi yake yakienda juu kimo cha mita 25.

Rais Donald Trump ametangaza hali ya hatari katika maeneo ya Kaskazini na kusini mwa jimbo la Carolina ambapo pia eneo kubwa la Washington DC limechukua pia tahadhali.

Kimbunga hicho kinachotajwa kibaya kuwahi kutokea siku ya ijumaa kinatarajiwa kuyapiga maeneo ya pwani ya mashariki.

Kutokana hali hiyo kwa sasa kuna msongamano wa magari barabarani,baada ya zaidi ya watu milioni moja kuamriwa kuyahama makazi yao. Matt Mardell ni mkazi wa eneo la Walterboro,kusini mwa Carolina.

”Kimbunga kingine kijulikanacho kama Matthew mwaka 2016 kiliangusha miti mikubwa juu ya farasi wetu,sema ilikuwa bahati ni kwamba dakika za mwisho,tulipewa tahadhali ya kutoka ndani ya nyumba zetu na kwenda maeneo salama,miti ilidondokea chumba cha kulala mwanangu wa miaka miwili,tulipata somo wakati ule.

Na unajua kulikuwa na upepo fulani hivi,leo wakati kimbunga hicho kikielekea Wilmington.Lakini tupo umbali wa maili kadhaa kusini mwa eneo hilo.Kwa wale waoga wanaanza kuondoka taratibu kwa uoogopa madhara ,lakini wachache wetu tumeanza kurejea kwa kuwa tupo maili mamia naa kusini.”anasema Matt Mardel

Hapo jana kwa nyakati tofauti jimbo la ,Georgia lilitangaza hali ya tahadhali,ikifuatiwa na CAROLINA,Virinia ,Maryland na Washington DC

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *