Home / Habari za Kimataifa / Kofi Annan: Katibu mkuu wa zamani wa UN azikwa Accra, Ghana

Kofi Annan: Katibu mkuu wa zamani wa UN azikwa Accra, Ghana

Ibada ya mazishi ya aliyekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan inafanyika katika mji mkuu wa Ghana, Accra.

Waombolezaji waliovaa nguo nyeusi na nyekundu wamejaa katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa mjini Accra ambako unaweza kupokea takriban watu 4000.

Watu wengine zaidi wamekaa katika ukumbi mwingine nje ya ukumbi mkuu wakitazama kupitia televisheni shughuli zinavyoendelea.

Wageni waheshimiwa kutoka kote duniani wanahudhuria mazishi ya kiongozi huyo wa zamani wa Umoja wamataifa akiwemo rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast pamoja na katibu mkuu wa sasa Antonio Gutterrez.

Viongozi wa kitamaduni, walizunguka jeneza la Annan

Waombolezaji wamekuwa wakiimba nyimbo na kumkumbuka Annan akiwemo mkewe, wakili nchini Sweden Nane Maria Annan.

Katika hotuba yake, ameeleza jinsi Annan daima alivyotazamia kurudi nyumbani, na ameishukuru Ghana kwa kumleta duniani mtu wa aina yake.

Alimaliza kwa kusema: “Ataendelea kukumbukwa kupitia wakfu wake na kupitia kwetu sote.”

Katibu mkuu wa sasa wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amewaambia waombolezaji, wakiwemo baadhi ya viongozi wa Afrika na viongozi wa zamani kwamba wakati Annan akizungumza:

Nukuu ya ujumbe huo: ”Dunia hutegemea kusikiza na tulifaidika kutokana na busara yake.”

Kwa muda wa siku mbili zilizopita mwili wake Annan umekuwa ukiagwa mjini humo na watu mbalimbali, wakiwemo watu maarufu.

Viongozi tofuati duniani wanahudhuria mazishi hayo katika makaburi ya jeshi ya Kambi ya Burma mjini Accra.

Mjane wa aliyekuwa rais wa kwanza afrika kusini Nelson Mandela – Bi Graca Machel na Gro Harlem Brundtland ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu nchini Norway ni miongoni mwa wanaohudhuria mazishi ya Annan

Mojawapo ni Graça Machel, mke wa aliyekuwa rais wa kwanza wa Afrika kusini, Nelson Mandela

Nukuu ya ujumbe wake: ”Daima alitetea amani , na kuwapatia watu kipa umbelekatika mchango wake duniani. Ninampenda kwa dhati, ni kakangu na kwa kweli nilazima niseme, bado sijakubali kwamba ameondoka.”

Kofi Annan alihudumu kama Katibu Mkuu wa saba wa Umoja wa Mataifa kati ya 1997 na 2006.

Leo inahitimisha kilele cha wiki kadhaa ya maandalizi ya mazishi yake, ambaye ni mmoja wa wana diplomasia wanaoheshimika duniani.

Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Accra anasema kuwa, ngoma za maombolezo zilisikika mfululizo kwa muda wa siku mbili katika Ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Accra, sehemu ambayo mwili wake ulikuwa ukiagwa na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Wachezaji ngoma wa jamii ya Ashanti wakati wa ibada iliyofanyika Jumatano

Miongoni mwa waombolezaji hao ambaye tayari amewasili mjini humo ni aliyewahi kuwa mke wa Rais wa kwanza wa Afrika kusini Nelson Mandela, Bibi Graca Machel.

Marais na viongozi kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika ikiwemo Ivory Coast, Ethiopia na Zimbabwe watahudhuria shughuli hizo za mazishi, wakiwemo pia marais wa zamani kutoka nchi za Ujerumani, Finland na Uswizi.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *