Home / Michezo / Rais wa Liberia George Weah acheza mechi ya kirafiki akiwa miaka 51

Rais wa Liberia George Weah acheza mechi ya kirafiki akiwa miaka 51


George Weah alichezea Monaco, Paris St-Germain na AC Milan – akikaa muda mfupi Chelsea na Manchester City

Rais wa Liberia George Weah alicheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kwa nchi yake siku ya Jumanne akiwa na miaka 51.

Weah ambaye ni mchezaji wa kwanza wa soka kutoka Afrika kushinda tuzo la mchezaji bora wa Fifa, alicheza dakika 79 kwenye mechi ambapo walishindwa na Nigeria kwa mabao 2-1 nyumbani Monrovia.

Liberia ilipanga mechi hiyo ya kirafiki kupumzisha shati namba 14 ambalo lilitumiwa na Weah wakati wa kilele cha taaluma yake.

George Weah alichezea Monaco, Paris St-Germain na AC Milan – akikaa muda mfupi Chelsea na Manchester City

Mchezaji huyo wa zamani wa AC Milan, ambaye aliapishwa kuwa Rais mwezi Januari, alishangiliwa wakati akitolewa uwanjani wakati wa mabadiliko.

Nigeria ilikuwa na kikosi kikali akiwemo Wilfred Ndidi wa Leicester na mwenzake Peter Etebo wa Stoke City.

Etebo alipiga kona ambayo Simeon Nwankwo aliitumia kuiweka Nigeria kifua mbele kwa mabao 2-0 baada ya Henry Onyekuru ambaye yuko kwa mkopo huko Galatasaray kutoka Everton kufunga bao la kwanza. Liberia walifunga bao lao kwa njia ya penalti iliyopigwa na Kpah Sherman.

George Weah alichezea Monaco, Paris St-Germain na AC Milan – akikaa muda mfupi Chelsea na Manchester City

 

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *