Home / Michezo / Benitez na Pellegrini – mameneja nyota waliojipata wakivuta mkia katika ligi

Benitez na Pellegrini – mameneja nyota waliojipata wakivuta mkia katika ligi


Rafa Benitez na Manuel Pellegrini

Rafael Benitez and Manuel Pellegrini ni mameneja wawili ambao walikuwa wamezoea maisha ya hadhi ya juu, lakini ambao sasa wamejipata mkiani katika timu tatu za mwisho katika Ligi ya Premio wakiwa na Newcastle na West Ham baada ya mwanzo duni katika msimu.

Benitez alishinda Ligi ya Mabingwa akiwa na Liverpool mwaka 2005. pia amekusanya vikombe vya Ulaya akiwa na Valencia na Chelsea huku naye Pellegrini akishinda kombe la Premio na Manchester City.

Hivyo ni kwa njia gani mameneja hao wawili wenye ujuzi wa juu wanaweza kushughulikia matatizo yao na wanawezaje kuziongoza Newcastle na WestHam kuelea?

Ni kwa nini mameneja hawa wawili wamejipata katika hali ngumu?

Newcastle bila shaka wamekuwa na wakati mgumu wakicheza mechi za nyumbani za Tottenham na Chelsea ni ile ya ugenini na Manchester City. Wakati mmoja wangeweza kupata ushindi ni wakati Kenedy alikosa penalti dakika za 96 huko Cardiff.

Tatizo la Benitez ni ukosefu wa mabao. Upande wa mhispania huyo umefunga mabao matatu tu kwenye mechi nne licha ya kutua kwake Salomon Randon kutoka West Brom.

Mkiani West Ham hawana pointi baada ya mechi nne.

Manuel Pellegrini na Rafa Benitez

Wanaokoselewa zaidi ni wachezaji kama Jack Wilshere na Mark Noble wachezaji wa kati ambao hawana nguvu za kutimiza mbinu za kushambulia za Pellegrini au kukabiliana na wapinzani wakati wanashambulia.

West Ham walionyesha matumaini walipocheza na Arsenal licha ya kushindwa lakini wakapata kipigo kikali walipocheza huko Livepool, na wakapoteza vibaya nyumbani kwa Bournemouth na Wolves.

Ni nani ataruka kuzuizi?

Siku ya Jumapili West Ham wataelekea Everton, eneo ambalo tangu jadi sio salama kwao wakiwa na matumaini ya kuzuia kuweka historia mbaya.

Everton hawajawai kupoteza mechi zao tano za kwanza za ligi.

Newcastle wanakabiliana na mtihami mgumu nyumbani na Arsenal lakini wanaweza kuwa na matumaini kuwa licha ya kupoteza kwa Spurs, Chelsea na Manchester City, mwanya wa kushindwa umekuwa mdogo kwa kati ya mabao 2-1 kwa kila mechi.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *